Vijana tunakosea wapi kwa maandalizi ya uzeeni?

Vijana tunakosea wapi kwa maandalizi ya uzeeni?

mrregion

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Posts
464
Reaction score
544
Katika maisha ya mwanadamu hupitia hatua kuu tatu nazo ni kuzaliwa upo chini ya wazazi, kuna hatua ya kuoa maamzi yapo na familia yako na mwisho ni uzee na kifo japo haujulikani utaishi miaka mingapi.

Usipowekeza utazeeka vibaya na watoto watakuchukua sana kwa vile watapitia maisha magumu ya kukulea na ukifa utakuwa umekufa bila kuwa na historia njema kwa familia na Jamii kwa ujumla.

Katika kuwekeza kuna mambo kadhaaa huzingatiwa ikiwa ni pamoja na kuwa mtiifu katika uwekezaji. Kwanza kabisa kuwekeza kwenye elimu kwa watoto wako, pili kuwekeza kwenye biashara short term project and medium term project, lakini pia kuna uwekezaji wa mda mrefu kabisa long term project.

Hapa nitaongelea sana kwenye long term project ila sitasahau na uwekezaji wa mda mfupi na ule wa mda wa kati.

Uwekezaji wa mda mrefu mara nyingi watu wengi huogopa kwa vile kwa mda wote huwa ni liability na sio asset nikimaanisha unatumia tu pesa bila kuingiza ila ipo siku itakulipa. Kwa tunaotokea mikoa ya nyanda za juu kusini kuna kilimo cha miti ambacho hutumia gharama kidogo kuendesha ila hadi uvune inachukua miaka zaidi ya 7 lakini pia unaweza kuuza hata kabla ya hapo. Kilimo hicho kimawatoa wengi hasa Iringa na Njombe. Nashauri vijana mwenzangu kulingana na mikoa tutokayo ni vyema ile ardhi ya urithi au ya familia tukawekeze kwenye biashara za mda mrefu kulingana na eneo au mkoa husika upo favourable kwa kitu gani.

Uwekezaji wa mda mfupi ni biashara ambayo mda wote inaingiza na tuliowengi tumezaliwa kwenye hizo familia, biashara za migahawa, maduka, nk. Biashara hii ni zuri ila yafuatayo yasingetiwe.

1. Mshirikishe sana mke wako kuiendesha ili siku ukitoweka iweze kuendelea na kulea watoto.

2. Usitegemee tu hiyo biashara endelea kutafuta zaidi ndo maana nimesema mshirikishe mkeo ili unapotafuta vyanzo vingine mke aendeshe. Nasema hivi kwa vile ukitegemea biashara hiyo tu utafeli maana unapata faidi tsh 5000 unakula 6000 kwa siku.

3. Biashara bila kuwa bahili hainogi sana, hapa ieleweke kuwa simaanishi usile hapana ila matumizi yasiyo ya lazima yaepukwe, wanaume hatukosi michepuko hivyo usijechukua hela ya biashara ukaendea bar au gest utafilisika vibaya sana.

4. Ni vyema sana tena sana watoto wako wakashiriki katika kuitunza hiyo biashara na usikose kuwaelimisha faida na matumizi sahihi ya pesa inayopatikana. Kuna mzee mmoja alikuwa na duka lake ila watoto hawakuruhusiwa kuingia dukani hivyo walikuwa wakivizia na kuingia na kuiba pesa na kuzificha chooni, bahati mbaya choo ilidondoka akaitwa fundi wakati fundi akiondoa udongo alikutana na pesa nyingi sana iliyokuwa imefukiwa hivyo alifaidi matunda ya wizi wa watoto kisa mzazi hukuwapa elimu wanao.

Biashara ya mda wa kati midterm project, biashara hii matunda yake huchukua miaka 3-6 kula matunda na mara nyingi wengi huwekeza kwenye elimu, ninaposema elimu namaanisha elimu kuanzia shule ya msingi na ikipendeza hata chuo kikuu.

Mzazi mwelewa na anajua anafanya nini huwekeza sana kwenye elimu na mda mwingi hupendi kuwa na watoto wake kuwapa motisha wa kusoma sana na kuwatabiria makubwa, mfano kama mtoto wake ni binti basi atamwambia soma sana uje uwe kama mama Samia makamu wa rais au naibu spika wa bunge, au Halima mdee nk na kwa mtoto wa kiume hivyo hivyo utamwambia akisoma sana atakuwa rais au mbunge kama Zitto nk.

Mwisho niwaombe vijana tuwekeze katika miradi mbalimbali hasa huko mikoani tulikotokea ili siku ujivunie kuzeeka kwako sio ujutie kuzeeka kwako.

Niwatakie mchana mwema mimi nimeamka tangu mwaka 2011 basi nawe amka kafanye uwekezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa sana tu, ngoja nianze. Ila kuna makabila ukiendelea tu kibiashara ndo tiketi yako ya kufa. Mke anakuua kisa wanaamini mwanaume akipata hela atatafuta michepuko na kupelekea kufilisika na watoto kupata taabu.

Barafu la moto
 
Nimekuelewa sana tu, ngoja nianze. Ila kuna makabila ukiendelea tu kibiashara ndo tiketi yako ya kufa. Mke anakuua kisa wanaamini mwanaume akipata hela atatafuta michepuko na kupelekea kufilisika na watoto kupata taabu.

Barafu la moto
Ni kweli but forget about it wekeza tu na cha msingi mshirikishe na unapofanikiwa usilete dharau kwa mkeo.

Mwanaume bora hata akiwa na mchepuko mzuri kiasi gani huheshimu sana mke wake wa ndoa na huwa wanatimiza wajibu ipasavyo nyumbani, ndo maana mme kama anatimiza wajibu nyumbani bila dharau hata awe kicheche vipi mke wake hawezi kuamini labda kwa kuona ila kwa maneno tu haiwezekani ila ukianza kubadilika na kuleta dharau mke hujiongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli but forget about it wekeza tu na cha msingi mshirikishe na unapofanikiwa usilete dharau kwa mkeo.

Mwanaume bora hata akiwa na mchepuko mzuri kiasi gani huheshimu sana mke wake wa ndoa na huwa wanatimiza wajibu ipasavyo nyumbani, ndo maana mme kama anatimiza wajibu nyumbani bila dharau hata awe kicheche vipi mke wake hawezi kuamini labda kwa kuona ila kwa maneno tu haiwezekani ila ukianza kubadilika na kuleta dharau mke hujiongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
Mke Mnyakyusa + Mchaga mmachame

Barafu la moto
 
Back
Top Bottom