Vijana tukumbushane kidogo

Vijana tukumbushane kidogo

point zero

Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
32
Reaction score
34
Ndugu zangu leo napenda niwakumbushe vijana wote tuliotoka kijijini na kwenda kutafuta maisha mjini

Tumekuja mjini kutafuta maisha tumewaacha wazazi wetu katka hali ngumu ya umaskini na ufukala

Nguvu zao zimewaishia kwa ajili ya umri na kututafutia sisi chakura na maradhi tulipokua watoto

Hivyo basi ni wajibu wetu sisi Sasa kuwatunza kwa chochote tukipatacho kiwe kikubwa au kidogo

Siku hizi vijiji vingi simu za mkononi zimefika unaweza kuwafanyia hata miamala ya fedha kupitia simu nao wakapata pesa kidogo kwaajili ya mahitaji yao

Wazazi hawa hawahitaji mambo makubwaa kama tunavyofikiri
Lahasha!! Wao wanaridhika kwa chochote kile kutoka kwa mtoto wao

kuna wakati wanaridhika hata kuisikia sauti yako tu hebu tizama ni pendo la namna gani hili!!

Ikiwa utaweza kuwatumia cash elf 5,000/= basi watatoa cash sh 3500/=

Pesa hiyo kwako ni ndogo sana na ndio maana unaizarau unaiona haitoshi ila kwao ni nyingi mno

3500/= wataweza kununua sabuni ya kipande, mafuta ya kupaka, chumvi, kiberìti na chenchi kidogo inabaki ya kununulia panadol

Rafiki maombi ya wazazi hawa juu yako ni mibaraka mikubwa sana maana mungu alituapia na kusema waheshimu baba yako na mama yako siku zako zipate kua nyingi na heri duniani

Hivyo nawasihii tuwakumbuke na kuwatunza wazazi wetu ili heri za mungu ziwe juu yetu.

Nawakilisha

20190512_133009.jpeg
 
Attachments

  • 20190512_133009.jpeg
    20190512_133009.jpeg
    144 KB · Views: 20
Kweli mkuu...unakuta mtu katoka kijijini , kafika mjini katusua anaanza kula mabia na malaya...anasahau..bibi..shangazi, mjomba, baba, mama, na ndugu wengine...Kuna papaa mmoja hapo Darisalama alikuwa anagawa pesa kama uchafu...watu walivoenda kumtembelea maza ake bush walikuta anachuma mchicha ulioota nyuma ya choo cha makuti.ndo anapika ili ale..
 
Inauma sanaa

Back
Top Bottom