Vijana tuishi ndani ya mambo haya manne

Vijana tuishi ndani ya mambo haya manne

East life

Member
Joined
Mar 26, 2021
Posts
43
Reaction score
47
Nawasalimu kwa salamu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania. kabla sijakwenda kwenye uzi wangu Napenda kuruhusu kuchangia

Nianze kwa kusema vijana ndio nguvu ya mataifa yote duniani. Kwa maana hii utegemeze na nguvu ya taifa inaangaliwa na vijana lakini inasikitisha kuona sasa vijana wengi tumekuwa tunazitegema na kudondoshewa mzigo wa lawana na chuki baina ya wenyewe kwa wenyewe familia pia hata taifa. Ni muda wako kijana kufanya maamuzi na kuishi ndani ya mambo haya manne yafutayo.


A: IMANI
Vijana wengi wa sasa imani zetu Zinalega lega kama tawi lililo katwa Na kutaka kuachia mtini. IMANi ndio Nguzo ya mwanaadamu. Nguzo hii Iweke kila sehemu yani amini kuwa Mungu yupo ana anaona kila Unachokifanya kila unalolifikiria kila Kinachokuja. Amini kuna changamoto na utatuzi upo na si kukimbia Changamoto zak😵ndoa mawazo Dhaivu kama ushirikina ,wizi na Thuluma. Jenga tabia ya kusali na Kumtegemea mungu kwa kila Unachokifanya iwe biashara, shule Kazi nk.


B: MATENDO NA KAULI
Ukiangalia dunia ilipo kwa sasa Mzigo mkubwa wa dhambi tunaubeba sisi vijana. Tumekuwa na uraibu Wa pombe,uzinzi,uvutaji,wizi,dharau nk. Kiukweli haya ndio Yanachelewasha maendeleo yetu na kuturudisha nyuma kivifikra hata Hekima na busara. Hili linatokana na
Kuiga tabia tofauti na maisha ya Wengine. kuishi ndani ya matendo na kauli nzuri kutatufanya Tujenge Heshima na thamani katika jamii Yetu pia kutuepusha na dhambi.
Waswahili wanasema ishi na watu Vizuri utaona matunda yake.

C: UBUNiFU
Wimbi kubwa la vijana tumekuwa Wavivu wa kubuni.Tumekuwa tukiwawaza misharaha na bata zisizo na Ulazima hatuna muda wa kupumzika na kusoma pia kufikiria na kubuni iwe
Kazini, biashara ama shuleni. Pia tunasaau kufikiria kuisaidia jamii Inayokuzunguka kwa mawazo, kifeza Ama miradi mbalimbali. Hivyo basi Ubunifu ni dira ya maendeleo ya
Binafsi na jamanii tujenge tabia ya kubuni


D: UAMINiFU
Hakika hapa ndipo kwenye kazi kwa Sasa kupata vijana wamini ni chang-
Amoto sana. Nafsi zetu zimegubikwa na tamaa za maisha mazuri ya haraka, pesa nyingi na madaraka haya Yanapelekea kuwa na imani dhaifu Na kishindwa kulinda mali za watu
Kudhulumu haki pia kutominiwa Jenga cha halali ,kula cha halali pia Ishi ndani ya ukweli wa maisha yako. Penda tabia ya kulinda bila kudokoa Mali za wengine.


NB: ukiishi ndani ya mambo haya Utakuwa mwenye amani na mwenye kuridhika na kila jambo
 
Back
Top Bottom