Vijana tuamke

Vijana tuamke

kensh

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
527
Reaction score
113
kuna mambo ambayo vijana tunapaswa kuyatafakari na kuyaamua kwa kutumia kichwa cha juu na si cha chini.vijana tumekuwa tukisota katika kutafuta mkate wa kila siku na ktk jitihada hizo,wengine wengi wamegeuka na kuwa tatizo katika jamii.wamekuwa wezi,majambazi na tishio kwa wengine.

kuna wale waliojaribu kuingia katika siasa ili kubadili maisha yao na wakwao,na wale walioingia katika siasa ili kujenga taifa lenye afya.wale wenye nia ya kushibisha matumbo yao,wamekuwa wasalitisi,wenye tamaa ya kupata,waongo na wenye kuwatumia vijana wenzao katika kufanikisha uovu huu kisha kuwalipa vijana hao ujira ili wawadhulu wengine wenye mawazo tofauti.vijana wamekubali kutumika na wanatumiwa kudhulu watu wa jamii yao.

wale wenye nia ya kujenga taifa,wamekuwa tunu,wenye utulivu wa akili na waungwana,ila kwa bahati mbaya,wamekuwa wakionwa kama wakupuuzwa pale wanapoibua mambo ya msingi kwa taifa.wengi wa hawa,wamesema waziwazi jinsi baadhi ya watu wanavyohujumu taifa,na hata vielelezo wameonesha,ila wamepingwa na kudhalauliwa na vijana wanaotumika kuhujumu vijana wenzao.

wazee ni muhimu,ila mawazo yao yanatakiwa kuwekwa ktk vitendo na vijana.kuna wazee wa hovyo pia wanaotumia vijana kufanya mambo ya hovyo,tuwakatae.tukiishia kushabikia siasa za vyama na kukosa maono ya kulikwamua taifa,tutaendelea kuliua taifa hili na hatimaye kulizika kabisa,yaani kulipoteza taifa letu na sis kuwa wachukuzi(porters) hapahapa tanzania.
 
Back
Top Bottom