Vijana sio wavivu, wala sio wazembe

Vijana sio wavivu, wala sio wazembe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Nakataa! Hawa sio wavivu, wamejituma kwenye kilimo, kiliwapora mitaji yao kwa ukosefu wa masoko na sera nzuri za kuwalinda wakulima, wafanye nini? Kwanza hata wakifanya kilimo hawafanyi kilimo kama wakulima (farmers) bali wao huwa peasnats tu, ambao hawawezi kupata faida kwenye kilimo hicho. Wakulima mnawajua kina Sumry au kina Masanja na wengine.

Hao siyo wavivu kwa kuwa wanajua wakikamatwa maisha yao yataishia jela lakini they take the risk anyway. Ndiyo wale wakiona gari ya mafuta imepinduka hawezi kuikimbia bali huikimbilia ili kupata namna ya kunusuru maisha yao. Hawa sio wavivu.

Kuna haja ya serikali kuangalia upya sera za vijana na ajira, ila kikubwa nilishawahi kusema, kwanza kuwe na marketing kubwa ya ile mikopo ya halmashauri na PTF, na masharti ya mikopo yabadilishwe ili kuleta tija kwa vijana wanaoweza kujiajiri ili wawaajiri na wengine.

Kama wimbi hili la vijana litabaki mtaani kama ilivyo hivi sasa, nadhani miaka si mingi ijayo tutaanza kuongeza majengo ya magereza kwa kuwa wafungwa watakuwa wengi.

Tuwatazame vijana.
 
Sio hivyo tu anayesema wajiajiri 'ameajiriwa' pathetic!!!
 
Kiukweli elimu sio chanzo cha vijana kushindwa kujiajiri bali hakuna mazingira rafiki, vijana hawana mitaji ya kukimu miradi au biashara (nazungumzia mtaji zimamoto) na pia biashara ni maarifa na sio elimu.

Pia viongozi wa kitaifa wajue kwamba isitafsilike eti wazo la mwisho kwa vijana waliohitimu vyuo vikuu ni kujiajiri.
Wanasahau kuwa hakuna mtu duniani aliyemsomi aliyefungua au kuanzisha biashara za kushauriwa au kupata shinikizo la kujiajiri.

Hapa duniani wapo wanaopenda kuwatumikia wengine (kuajiriwa) yaani wanapenda na wapo wanaopenda kuajiri wengine (kutumikiwa) yaani wanapenda kuwaza kujiajiri sasa msiwachanganye katika kapu moja.

My word to you!
"Business is knowledge no matter who are you, please respect any kind of business in your town"
 
Back
Top Bottom