Vijana Njooni CCM, ndoto zenu zitatimia

Vijana Njooni CCM,

Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina "Sera ya malezi ya Vijana" iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.

Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.

Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.

Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.

Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!

Hizi picha hapa chini zinaonyesha uhalisia wa Vijana wa CCM wanavyotumika je unataka waje wayafanye haya huko CCM au waje kufanya nini?

View attachment 144452 View attachment 144453 View attachment 144454 View attachment 144455 Green Guard.jpg View attachment 144457 mwigulu WDC.jpeg View attachment 144459 View attachment 144460
 
Ni heri nipigwe risasi ya kichwa na nife kuliko kuwa mwanachama wa CCM...kwani CCM ni chukizo hata kwa Mungu! Na alaaniwe kila anayesababisha uwepo wa CCM na viongozi wake hapa Duniani ikiwemo wewe Makonda.
 
kwani miaka yote vijana walikuwa wapi kama si ndani ya CCM inayoongoza nchi hii tangu uhuru na je kwa nini ndoto zao bado ni giza totoro? Ushauri wangu kwa vijana ambao tumeshaona nuru basi tuikimbilie huko huko iliko lakini kuendelea kuwa ndani ya CCM ni sawa na kukubali kuendelea kujifunika blanketi jeusi wakati kumeshakucha kitambo!!

Mimi huwa najiuliza sana! hii sera ya vijana ni taifa la kesho inamaanisha nini hasa!!? tokea uhuru hawa vijana bado wanasubiria kesho tu?? na waliosubiria hiyo kesho bado ni vijana au ni vikongwe?? kweli sasa naamini uwongo humtetea mtu kwa kitambo tu na kisha kumuacha uchi wa aibu! CCM huo uongo kila mtu anaujua kwa sasa na hata mlio wa hadaa kuwa kesho watakuwa Taifa leo hii wanakufa kwa kukosa kuthaminiwa na ninyi mlio aminiwa nao (Ni wazee sana na wanaishi kwenye makambi ya wazee kwa mlo mmoja tu tena duni), mbona mnayo hubiri kuwa ni sera ya CCM ni ardhi na Mbingu kimatendo? na nikwanini mnaona ni sawa tu kulaumiwa na watanzania? HII DHAMBI HAITA WAACHA, na ni laiti mngejua ni bora kuanza kulia umalize kwa kucheka kuliko uanze kwa kucheka umalize kwa kulia.
Haya ngoja tuone MUNGU atatutetea kwa njia ipi kwani kulipa visasi ni kaze yake MUNGU
 
kweli ccm ya wazee hilo linathibitishwa na kuwapa nafasi vijana wasio na nidhamu kwa jina la trial and errors,na ukimwona kijana ccm fahamu ya kuwa ni mtoto wa kiongozi wa ccm au ana biashara eneo la barabara (kimaslai zaidi
 
Labda vijana wenye mtindio na ulemavu wa akili kama vile Juliana Shonza na Mtela Mwampamba ndo watakuwa wamekuelewa.
Bila kuwasahu wale mateja kutwa kuchwa kukwapulia watu simu zao.
 
Last edited by a moderator:
Aheri ungesema twende kwa Mungu. CCM Sio kitu Mbele Za Mungu Yehova. Hivyo utuase twende kwa Mungu na si CCM ili ndoto zetu vijana zitimie.
 
Vijana Njooni CCM,

Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!

Makonda,

Kwanza nikupongeze maana walau umejipambua kuwa mpambanaji na mtetezi wa CCM kwa hoja zenye tija sio kama vijana wengine wa CCM wasioweza kutofautisha masuala na kupambana na haiba za watu.

Pengine style yako ya kuipambania CCM itainusuru CCM inayoendelea kupoteza mvuto kwa vijana. Nikutakie kila la kheri kwenye uthubutu wako huu.

btw, ni lini salamu za umoja wa vijana wa CCM zimebadilika toka Wa Wii ama Wiii Waaa kwenda Vivaaaa Vijana Vivaaa?
 
Ooh salale sasa wewe ndio umekuwa mwerevu sio?

Hebu niambie huyu aligombea kwa hiyari yake? Hadi mke akaingia ulingoni kumuokolea jahazi? Baba mkwe naye pia akaingia? Si Lusinde alisema tumchague ili asaidie familia ya marehemu babab yake kwa maposho atayo yapata? Baba yake angekuwa mvuvi angeacha kazi bank akavue samaki?

4.jpg

Umenena vyema sana mkuu,nashukuru Mungu bado tuna vijana wenye busara kama wewe hapa tz
 
Vijana Njooni CCM,

Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina “Sera ya malezi ya Vijana” iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.

Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.

Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.

Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.

Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!

Asante sana comrade
 
Kati ya dhambi zisizo samehewa kwa Mungu ni kujiunga na CCM,chama kinamshirikisha hadi Mungu kwenye ugaidi..
Cc;Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom