Vijana Njooni CCM, ndoto zenu zitatimia

Kwa akili zako hizo Sina budi kusema Ni kweli hata chuo uli disqualify. Na pia huko CCM labda watu wafuate utajiri WA kuuza unga kama WA kwako na kubobea kwa kwa uboya kama ulivyo.
 
Vijana Njooni CCM,

Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina “Sera ya malezi ya Vijana” iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.

Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.

Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.

Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.

Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!

Well done bravo umefafanua vizuri .
 
Sasa nimekuelewa Makonda , wanaokulaumu kwa kutajirika bila maelezo hawakusoma uzi huu .
 
Naona Leo uko kwenye kampeni
Ukimaliza tafadhali njootutatulie kero ya usafiri
Tunapata tabu sana kuingia mawasiliano wakati wakuelekea Makumbusho
Ni kupoteza Muda na kuongeza stress.
barabara yenyewe ya kuingia mawasiliano ni mbovu.
@paulMakonda
 
Mbona vijana 3000 walioajiriwa na kupewa mikataba ndoto zao hazijatimia? Ccm ubabaishaji mtupu

Kwani hao 3000 ni wanaCCM??Amesema wanachama wa CCM rafiki.Ubaguzi wa kiwango cha lami unaoendelea sasa hivi.
 
Hivi leo kuna nini?
huu ni uzi watatu nauona wa paul makonda nani sijui anazifukua huko!

Kweli idumu #Jf
 
Binafsi siwesi kuja kumejaa unafiki na kasumba za uongozi wa kubebana kiukoo na kimaslahi ...

Juzi tu tumeshuhudia vijana haohao mnapishana kauli na kukosoana mbele ya vyombo vya habari ... na imeshatokea mara kadhaa ...

Ingekua ni kweli vijana mmelelewa katika maadili ya uongozi uliotukuka leo hii tusingekua tunazunguzia na kuhoji uhalali wa vyeti vya mtu au kutaka kujua historia ya mtu kielimu na kiuchumi ... ilituweze kupata ushahidi wa shutuma za mtu juu ya matendo yake yasiyo pendeza kama kiongozi ...

Najua unafahamu mengi sana zaidi yangu ... ila nikwambie kitu "Chama Chetu Mizigo" ... kimekua kinaendeshwa na misingi ya kasumba ya kutukuza waanzilishi au waliotangulia ... kwa hiyo maadili ya uongozi ndani ya chama yana egemea katika nguvu ya msingi wa aliye kusababisha uwepo hapo ulipo kama kijana ...

Hao woote waliotolewa mfano ni watoto wa makada waliokua na nafasi zao za kibabe ndani ya chama ... nankama sio mtoto wa kada fulani basi utakua uliishi chini ya kada fulani na kutimiza lengo lake katika kampeni yake fulani ... na hivyo utapewa shukurani kwa kufanywa kama kijana wa mfano ...

Hili tumeliona ... ndio maana leo hii umekua na sauti ya kiburi na majigambo pengine kushinda hata hao watoto wa makada ... na tokeo yake ikafikia kukosoana na kupigana vijembe mbele ya vyombo vya habari ... sasa jiulize zile ofisi za nini? Eti massage sent ... kwani ulimlenga nani? ... kama kweli wameandaliwa kuwa viongozi bora si mngeitana katika ofisi zenu na kunyooshana vizuri leo hii mnanyooshana mbele ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii tena kwa vijembe na majungu ...

Leo hii tunashuhudia kiongozi anaejiita kaandaliwa kwa maadili ... imefikia anatoa kauli za dharau mbele hao wazazi wake walio muandaa na wazazi wanachekelea ... Hii ni sawa na mtoto aliye mtukana jirani yako halafu kisha unamsifu mwanao kuwa ni shujaa na jemedari na hana mzaha ... kweli jamani?

Hebu tijiulize huyo January, Nape, Jerry ni watoto wa kina nani ndani ya CCM ... na huyo Sugu, Lema, Mdee ni watoto wa kina nani ndani ya Chadema?

Leo hii huyu unajiona kuwa wewe ninmteule kutokana na kuiva kimaadili ndani ya Chama kama kijana ... anasahau kua uteule wako ni shukrani ya kulinda maslahi ya makada fulani ndani ya Chama ... kwani unafikiri sisi hatijui yaliyojiri kutokana na mgogoro uliopo katika ya CCM na kigoda cha mwalimu?

Leo hii kijana mwenye maadili angekwenda kuvuruga mkutano wa Mzee warioba ... na wewe kama wewe usingeweza ila ni kwa sababu kapewa baraka na hao waliomuweka pale ... na ukae akijua bila ya hilo hakuna ambae angekufahamu ungebaki kua kihelehele na meneja wa kampeni za Chama Kwisha ...

Mwisho kabisa napenda nikwambie kua vijana ndani ya "Chama Chetu Mzigo" wanalelewa katika misingi ya kasumba kwa kuangalia na kwa kulinganisha uwepo wao na nguvu ya alie kusababisha uwepo hapo ulipo ... Upo hapo Mkuu
 
Vijana Njooni CCM,

Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Chama Cha Mapinduzi, pamoja na mambo mengine bora, kimetimia vyema katika muundo wake kwa kuwepo kwa jumuiya imara zinazoishikilia na kuipa nguvu kila Uchao. Ipo jumuiya ya Vijana ambayo lengo kuu la Kuundwa kwake ni kuhakikisha kuwa Chama na Taifa linaandaa na kulea Viongozi wake wa kesho. Ni chama cha Mapinduzi pekee miongoni mwa vyama vyetu vya siasa hapa nchini ambacho kina “Sera ya malezi ya Vijana” iliyotungwa tangu 1981 na kuendelea kufanyiwa review mpaka sasa.

Vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi wanamatumaini Zaidi na wanaandaliwa na kusafishiwa njia ya mafanikio yao kwa mapenzi na weledi wa Viongozi. Tabia hii ya viongozi wa CCM kuwaandaa Vijana makini na kuwatengezea mazingira kwa kuwalea na kuwadhibiti katika matendo na mienendo ndio ambayo inakihakikishia Chama hiki Uhai wa miaka mingine 50 na hata Dahari. Ni wazi leo ukiwaangalia Vijana ndani ya CCM unaona picha ya Viongozi bora wa kitaifa wa Miaka 20 ijayo, ukiomuona JANUARY, NAPE, JERRY, n.k unaona picha ya Viongozi bora wa baadae tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc unaona kiza na wingu zitto.

Tofauti na vyama vingine, CCM ukiwa kijana una-reside your right of trial and error, kwa maana tumeshuhudia Vijana wengi ambao walikosea lakini wanapewa nafasi na kuwa Viongozi wakubwa na wazuri baadae, mifano hii iko mingi, binafsi nimewahi kufanya makosa lakini niliitwa na kuonyeshwa njia, na nilifanyiwa hayo sio kwa sababu mimi ni msukuma ama ------, kwa sababu kwenye Chama Chetu Usukuma ama ukwere sio sifa ya kuwa kiongozi kwa maana sikuangaliwa kabila langu ili niadhibiwe ama nisamehewe. KABILA halimbebi mtu ndani ya CCM.

Ipo siku niliitwa na Mzee wangu KINGUNGE NGOMBALI na akawa ananifundisha darasa la ITIKADI, tukaendelea na mjadala nikamuuliza ameweza vipi kuwa kiongozi mkubwa na mwenye heshima ya kipekee ndani ya Chama hali yeye haamini katika DINI yeyote.,akanijibu kwa ufupi na ufasaha kuwa DINI ya mtu sio sifa ya kuwa KIONGOZI ndani ya CCM. Kwenye CCM kila kijana na kila kiongozi ana sifa sawa na wengine, hakuna aliye mbora mbele ya wenzake, vipo vigezo vinavyotumika kumpata kiongozi, sio lazima uwe PADRI ama MCHUNGAJI ndio uonekane unafaa kuwa kiongozi ndani ya Chama, kwetu sisi DINI ya mwanachama sio sifa ya kuwa bora kwa wengine.

Nitoe wito kwa Vijana wenzangu kuuona ukweli huu na kuufuata, ufike wakati Vijana wajiandae na waandaliwe kuwa Viongozi Bora wa Kizazi Chao. Njooni CCM ambako ndoto zenu zitatimia, michango, uwezo na mawazo yenu itathaminiwa. Njooni ambako mtaonyeshwa njia ambayo mtakuwa tayari kuifata.

MWENYEZI MUNGU AWABARIKI NA AWAONGOZE KATIKA NJIA YA SAWASAWA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa…!!!
Jamani vijana tujiulize hawa ... JANUARY, NAPE, JERRY, n.k ambao tunaambiwa tuone picha ya Viongozi bora wa baadae ... Je unafikiri ni watoto wa nani na Baba zao ni kina nani ndani ya CCM!!!??? tofauti na ukiangalia wenzetu SUGU, LEMA., NASSAR etc ambao tunaambiwa tuone kiza na wingu zitto ... Je, hawa ni watoto wa nani na Baba zao ni kina nani ndani ya CHADEMA!!!???

Hapo ukipata jibu utaona kua CCM ni chama chenye mfumo wa uongozi wa kasumba kwa Makada na familia zao au kwa maslahi yao kwani wao ndio wenye chama ... tofauti na CHADEMA ambao wana mfumo wa fursa kwa vijana ... take it brother
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom