Tanganyika jeki
JF-Expert Member
- Jun 12, 2011
- 243
- 87
Ni vizuri taifa wakati fulani lijikite ktk kujadili uongozi na viongozi wa taifa wa baadaye. Kwa miaka ya karibuni kuna vijana wajiandaa kushika uongozi wa juu wa nchi. Wachache wana vigezo stahiki. Baadhi ya vigezo ni uwajibikaji kwa wananchi, bidii, maarifa, uadilifu, na uzalendo. Je, kuna vigezo vya kiongozi bora zaidi ya hivyo? Je, kati ya Zitto, Makamba, J., Itatiro, Mdee, Nape, Mwigulu, Mnyika nani aweza kushika nafasi ipi kati ya urais, m/rais, m/mkuu? Je, kuna wengine zaidi ya hao?