MtazamoWangu
JF-Expert Member
- Apr 25, 2009
- 313
- 7
mhhhhh?jamani mbona tuna vijana wegi tu....watoto wengi wa viongozi wetu wapo kwenye nafasi tofauti tofauti za kisiasa..huenda hawa baadae wakaja pia kuwa viongozi wa juu wa nchi..lakini pia tunao vijana wengine pia wanao-onyesha interest na siasa...ngoja tuone 2010 watakaojitokeza,......
Hivi kumbe A.Mashariki ina nchi hizi..!
Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa kaajili ya nguvu walizo nazo zaidi, lakini si kwenye ngazi za juu za maaamuzi, MAANA HUKOWATAKOROGA.
Ni ukweli uliositirika kwamba maamuzi mengi ya vijana yana mwelekeo wa jazba na uharaka usio na maana!
Ukiamua kuingiza vijana kwenye ngazi za maamuzi, lazima wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.
Ukiona Mbunge kijana sana ujue kwamba amechaguliwa na kundi la vijana wenye hasira ya maisha, ambao wanadhani kijana mwenzao atawaelewa hatraka na kuwasaidia.
My take-
Vijana wawe groomed kushika nafasi za uongozi, na si kutoka masomoni au uraiani direct na kuwa viongozi. Mifano ni kama ya akina JK, ambao wamekulia kwenye Siasa!
Boramaisha,Si kweli!
Vijana wanaweza. Uongozi ni kipaji na wala mtu hapaswi kuwa groomed ndio awe kiongozi bora.
Vijana wenye kuonyesha uwezo wa uongozi hawana budi kugombea ili Taifa liwe na viongozi wengi vijana watakaotoa changamoto ya kweli kwa kuwa na mawazo mapya na nguvu mpya.
Hao wazee unaowaona katika siasa sasa hivi, walianza wakiwa vijana. Nadhani issue hapa si kwamba vijana hawahusishwi, pengine vijana wengi wa umri huo sasa hivi hawajihusishi na siasa.
Watu wanatafuta shibe mkuu...tatizo wote mnataka kujiunga na CCM.
..NCCR,TLP,UDP,CCJ, etc wapo wanawasubiri mjiunge nao.
Njia nyepesi...tatizo wote mnataka kujiunga na CCM.
..NCCR,TLP,UDP,CCJ, etc wapo wanawasubiri mjiunge nao.