REBEL
Senior Member
- Dec 15, 2010
- 166
- 65
Nimekuwa nikitafakari hali ya siasa na mchango wa vijana katika maendeleo ya Jamii.
Mungu amenijalia kutembelea maeneo mengi ya nchi yetu kama mji magharibi, Unguja kusini, Mwanza, Arusha, Bukoba, Iringa,dodoma n.k .Na wimbo ni ule ule kuwa vijana hawadhaminiwi kabisa.
Suala moja la kwanza ninalotaka kulizungumzia ni wamachinga. Kitendo cha maaskari wa mji/ jiji kuwar vijana kwa kuwaibia na kuwabughudhi wamachinga kunawarudisha nyuma kimaendeleo vijana. Kwa mfano mwezi uliopita hapa mji magharibi, Zanzibar serikali imeamua mji uwe msafi. Na wao walichoamua ni kuwa wafanyabiashara ndio wanaochafua mji na wakaanza kuwakamata na kuwaghasi.
swali :Je hii ni haki?
Na hili si tatizo la hapa zanzibar tu bali ni chanzo cha migogoro kote bara kuanzia Mbeya, Mwanza, Arusha na miji yote mikubwa.Ni imani yangu kuwa sheria inabidi zitungwe ili kuleta maendeleo kwa watu wake na kutambua sekta zisizo rasmi na sio kunyanyasa vijana.
Kitu cha pili, ni wimbi la vijana wasio na kazi walio wasomi na wasio wasomi linazidi kuongezeka. Hili ni bomu ambalo serikali inalikuza kama Lowassa alivyosema. Tatizo wizara ya kazi na yule waziri mwizi wa kura Prof. Makongoro Mahanga wa jimbo la segerea hajui kuimudu wizara yake yuko tu kuuza sura.Simpendi huyu wazirikabisa kazi kukaa tu ofisini.
Sema katika haya yote kuna vitu vinavyonipa matumaini kwa kuona vijana wanamudu siasa vyema sana sana wa NCCR- Mageuzi na ChaDEMA. Vijana hao ni Mkosamali, Kafulila, Machali, Mnyika, Lema, Silinde. Wengine ni Wenje, Halima Mdee, Regia Mtema na Sugu. Sema wakaze buti na Mungu atawasaidia. Vijana waliotuangusha ni yule katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye na yule zero Lusinde hata na Makamba January, na kingwangala hawako kwa ajili ya vijana na wanaboa.
Vijana tutetee haki zetu na katiba mpya.sio tu kila siku tunaimba mapenzi tu.
Nawasilisha.