Vijana na hatma ya nchi yao

Vijana na hatma ya nchi yao

shakelyie

Member
Joined
Jul 15, 2016
Posts
21
Reaction score
18
Tafiti katika nchi nyingi za kiafrika zimeendelea kuonyesha kuwa asilimia kubwa ya vijana hawashiriki katika mchakato mzima wa chaguzi za kisiasa kuanzia kujiandikisha katika madaftari ya kudumu Hadi kupiga kura.

Sababu nyingi zinatajwa na vijana wenyewe lakini sababu kuu mbili zilizonirudiarudia sana ni hizi:

1. Hawaamini kuwa ufumbuzi wa matatizo yao na ya kijamii umelala katika mikono ya siasa kwa kile wanachoeleza kwamba wanasiasa si watu wakweli na ajenda yao ni kuwatumia wananchi kupata uhalali wa kukalia ofisi za umma na kutekeleza ajenda zao wenyewe na vyama vyao.

2. Wagombea wengi katika nafasi za uchaguzi ni watu wa makamo. Hii inawapa tafsiri kwamba kundi Hilo halitakuwa na uwakilishi wa moja kwa moja wa matatizo na changamoto zao na hivyo hawaoni umuhimu wa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi kwa vile kwa vyovyote vile na kwa yeyote yule atakayeshinda au atakayeshindwa halitakuwa na mchango wowote au madhara kwa maisha yao baada ya uchaguzi

Walipoulizwa kwanini wasijitokeze na kugombea katika chaguzi ili kuwa na idadi kubwa ya wawakilishi watakaosukuma shida na changamoto zao katika ngazi za maamuzi wengi walitoa sababu zifuatazo:

1. Gharama za kuendesha kampeni za uchaguzi ni kubwa mno kwa kijana wa kawaida aliyehitimu masomo au wa kutoka familia ya kifukara kuweza kumudu!
Vijana wengi wanaoweza kuthubutu na kumudu ni wale waliobahatika kupata kazi zenye maslahi mazuri na kukusanya mtaji kwa miaka kadhaa

Wengine ni wale ambao familia zao zinajiweza na hivyo haiwawii Vigumu kuingia ulingoni na kushindana na wanasiasa wakongwe,wagombea watetezi wenye pensheni za mamilioni ya shilingi mifukoni.

2. Sababu ya pili ni ile ya kukosa jukwaa la kuanzia ! Wapo vijana wengi wenye uwezo mzuri wa kisiasa lakini hawana mahali pa kuanzia panapoweza kuwabeba na kuwatambulisha kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi ili kuwapa uwanja sawa wa kisiasa wa kuchuana na wenzao wa kutoka familia za kisiasa ambAzo baba au mama ni au alikuwa mbunge,waziri au Rais!

Kushindana na mwanasiasa mkongwe,mfanyabiashara tajiri au mwanafamila wa kigogo bila kuwa na historia Wala egemeo lolote ni kujipotezea muda.

Kwenya muziki na maeneo mengine kwa mfano kumekuwa na mashindano na majukwaa ya kuibua na kukuza vipaji ambapo yanawabeba wasanii na kuwaweka katika nafasi ambapo wanapata kufahamika na hata kualikwa na makapuni ya kufanya nao kazi baada ya kuwaona uwezo wao kwenye mashindano hayo.

hali haiko hivi kwenye siasa na mpaka kijana ajipenyeze na kujilikana uwezo wake kwa viongozi wa Chadema,CCM,act au cuf ni shughuli pevu inayokatisha tamaa.

Kwa mtazamo wako je unafikiri ni Nini kifanyike ili kuwatengenezea vijana mazingira rafiki ya kushiriki kwenye siasa kwa kugombea na si kulalalmika mitandaoni?
 
Back
Top Bottom