Vijana msikubali kutumika katika swala la katiba mpya:

....umenena mkuu,tatizo la vijana wengi wa sasa wanakosa kujiamini katika mustakabali wa maisha yao na kisha taifa kwa ujumla. wwengi wanadanganywa kwa maslahi ya watu wachache kwa kupewa ahadi na viposho vya hapa na pale. lakini kwa kijana anye jitambua kamwe hatafanya mambo ya kipuuzi kwa kukubali kutumika kama taka ngumu. kimsingi itafika wakati mabadiliko yatalazimisha wabadilike na kama hawata kubali system itawa phase out....
 
Ndugu wanajamvi, habari ya jumapili! nimeona leo tuweze kushare mada hii muhimu ikizingatiwa kuwa sisi sote ni wadau wa hatima ya taifa letu na si vinginevyo. Kumekuwa na tabia ya vijana wenzangu kutumika kisiasa katika mambo mbali mbali hususani ya kisiasa bila kujua hatima ya nini tunachokifanya. Kwa mfano ni sisi vijana ndio tunaoratibu mikutano mingi ya kisiasa moja kwa moja au kwa nyuma. Leo hii vijana tumefika mbali hasa katika swala la mchakato wa katiba mpya , kuna vijana wanajiita eti VIJANA WA CCM ELIMU YA JUU nimewaona kwenye TV wakipinga na kuhoji muungano wa viongozi wakuu wa vyama vya siasa kuhusu swala la katiba mpya, sasa mimi nawauliza ninyi vijana mnamasilahi gani katika mchakato huu? eti mnajinadi mnawakilisha vijana, vijana gani mnawawakilisha? na nani amewatuma? au mnatafuta umaarufu ili baadaye mpewe UDC na mambo yanayofanana na hayo? Kama hamuelewi vitu kaeni kimya ......njaa zenu zisiwaponze watanzania wengine. Kifupi ni kwamba sheria ya katiba mpya ni mbovu ndo maana tunamuomba mh; Rais asisaini huu mswaada kwa manufaa ya vizazi lukuki vijavyo,......Nyiye mnaita press conference na mashati yenu ya kijani eti mnawapinga viongozi hawa.....maana ya elimu ya juu wadogo zangu siyo hiyo mnayodhani ninyi....ila ni kuweza kutafakari mambo na kuwa msaada katika jamii inayokuzunguka kama wanavyofanya hawa viongozi wa siasa. Ari yangu ni kwamba tabia hiyo msirudie ,sisi vijana hatuwatambui ninyi katika swala la katiba ya taifa hili,......kama mnainterest zenu naomba namomba mkazifaniye kwenye mambo tofauti na hili........ kwasababu hamjui mlifanyalo tunawasamehe bure!

Heading ingependeza kama ungesema vijana wasitumike na wana magamba ungeeleweka vizuri
 
Back
Top Bottom