Kawe Alumni
JF-Expert Member
- Mar 20, 2019
- 8,685
- 11,988
Vijana wa kiafrica wamekuwa wahanga wakubwa na siasa za uchumia tumbo kwa Viongozi wa Africa wenye tamaa ya madaraka.
Kwa kuwa vijana Wengi wanakuwa wametoka vyuoni hawana mwelekeo wa maisha wanarubunika na kila fursa inayojitokeza mbele yao ili mradi wapate kushibisha tumbo.
Hali ambayo unawapelekea katika hatari pale wanapojikuta wamevunja sheria za Nchi na kuingia matatani.
Vijana wanakuwa wabeba mabegi wa Wanasiasa walaghai. Wanasiasa wao tayari wameshajijenga kiuchumi wengi wameficha mapesa nje ya Nchi, wengi wana visa mkononi akikosea anakimbilia nje ya Nchi anakuacheni nyie vijana mnaozea mahabusu.
Pia mwanasiasa akiona kesi uliyofanya inaweza kumuharibia jina kisiasa anakutelekeza mahabusu upambane na hali yako.
Wanasiasa wanakuwa wanagombana wanapokuwa wameshika maik wanahutubia tu,ila wengi nyuma ya pazia ni marafiki wanakunywa wain pamoja. Nyie mnaokesha mtandaoni kuwapigania mnapoteza muda muda tu.
Vijana mjifunze kwa Kabendera mslighaiwe na wanasiasa wasaliti wa Nchi yetu wenye tamaa ya madaraka mkipata matatizo mnatelekezwa mahabusu.
Vyama vingi vya upinzani Africa ni kwa ajili ya ujasiriamali na si kusaidia Mwananchi
Tuwakimbie hawa Wanasiasa waongo
Bahati nzuri tuna Rais anayeongoza bila kujali Chama cha mtu haina haja kukaa vyama vya upinzani