Katika vitu ambavyo havinaga komando, tajiri au gaidi ni mapenzi, ndiyo maana kuna baadhi ya watu huko nje ni wakali sana lakini wakifika kwa wake zao au waume zao wanakuwa wa pole sana.
Mapenzi yana nguvu sana vijana, kwahiyo tusidanganyane kuwa sijui mimi mwanamke kwangu hana nafasi au mwanaume kwangu hana nafasi. Mapenzi ni kitu ambacho kipo nature ni Mungu mwenyewe alikiweka.
Mwenzenu ukicheki mada zangu nyingi unaweza kufikiri labda mimi sijawahi kuumizwa na mwanamke, kwasababu ninavyojidai hakika utafikiri mimi ndiyo gaidi wa mapenzi lakini ukweli ni kwamba mwenzenu nimeshawahi kupigwa na kitu kizito kichwani kwasababu ya mapenzi.
Na siwezi kusema sitopenda tena eti kwasababu nimeshapigwa na kitu kizito, eti mapenzi hayana nafasi kwangu tena. Ndugu yangu labda nikutane na wale ambao siwapendi lakini nikikutana na yule ninayempenda kwa dhati, akitaka kuniumiza nitaumia kama mwanzo.
Cha kufanya ili kuepuka adhabu ya mapenzi ni kujigeuza, maana nasikia eti wale hawanaga hisia za mapenzi!