DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Wananchi wa Kahama Mkoani Shinyanga wakiwemo Maafisa usafirishaji wanaotumia Pikipiki na Bajaji, Mama Ntilie, Machinga na wapiga debe wamebainisha maandalizi yao katika ushiriki wa uchaguzi Mkuu wa Jumatano hii Oktoba 29, 2025, wakisisitiza umuhimu wa Vijana wenzao kutotumika kisiasa na kwa maslahi binafsi ya wachache wanaowahamasisha kufanya vurugu na maandamano siku ya Uchaguzi Mkuu.
Maafisa usafirishaji hao mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Frank Nkinda leo Jumatatu Oktoba 27, 2025, siku mbili tu kabla ya uchaguzi Mkuu, wamemuahidi Mkuu wa Wilaya kuwa mara baada ya kupiga kura watarejea Mtaani na kuendelea na shughuli za usafirishaji badala ya kukaa Vituoni ama kuingia Mitaani kuandamana kama ambavyo baadhi ya wenye nia ovu na amani na Maendeleo ya Tanzania wamekuwa wakiwataka kufanya hivyo ikiwa ni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi Mkuu.
"Hatutakubali kutumika, hatuandamani na Oktoba 29 tunaenda kutiki. Sisi kama Vijana wa bodaboda tumekubaliana kuwa hatuwezi kuingilia ugomvi tusioujua na hatuwezi kukubali kutumika kama mbuzi wa kafara. Wanaohamasisha uvunjifu wa amani wapo nje ya nchi, tukiathirika watabaki kwenye Mataifa yao na kutucheka." Amesema Haruna Muharami, Mmoja wa waendesha bodaboda hao.
Maafisa usafirishaji hao pia kwa umoja wao katika Vituo mbalimbali, wamemuahidi Mhe. Nkinda kuwa watakuwa mabalozi wa amani na usalama katika kipindi chote cha uchaguzi Mkuu na hata baada ya uchaguzi huo, wakisisitiza umuhimu wa kutoa taarifa kwa Viongozi pale ambapo watashuhudia dalili ama uvunjifu wowote wa amani katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Frank Nkinda amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaowataka bila ya kuwa na wasiwasi ama hofu yoyote, akiwahakikishia usalama na mazingira tulivu wakati wa upigaji wa kura na baada ya zoezi hilo, akionya wale wote wanaopanga ama kuratibu uvunjifu wa amani katika Wilaya hiyo katika kipindi hicho cha uchaguzi Mkuu wa Tanzania.