igp
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 839
- 543
Niwazi na kweli kwamba chadema kama chama cha siasa kimejinasibu kwa mda mrefu kuwa ni chama cha demokrasi lakini undani wake siyo kweli.Yapo mambo mengi ambayo yanaifanya chadema kuwa chama cha kundi flani la watu hasa wazee lakini vijana nafasi yao haipo ndani ya chadema,Vijana wachache waliopewa nafasi ndani ya chadema pengine ni wale tu ambao ni vibaraka wa wazee wa chama ndiyo hupata fulsa hiyo.Kijana ambaye hawezi kujipendekeza au kuwa kibaraka au kutumika na wakubwa kwa ile njia nyingine kamwe hawezi kupata nafasi hiyo,fuatilia utaniambia ukweli huu.