Uchaguzi 2020 Vijana hawana cha kupoteza kwa Dkt. John Pombe Magufuli

H

Hizo asilimia wala siyo Magufuli aliyeziweka,ukiwa muongo inabidi uwe na kumbukumbu hasa.Umewahi kufikiria huko Halmashauri wanayo hayo mapato ya kutolea mikopo?Hizo takwimu za idadi ya ajira zinaaminika kwa kiasi gani?NBS wamezithibitisha?
Hatudanganyike na hizi propaganda za CCM,kuna mambo mnamsifia nayo Rais wakati siyo mhusika wake na kwa kufanya hivyo mnamdhalilisha.
shida wanafikiri tupo zama vita baridi na propaganda labda kilichobakia ni kuiba kura nothing more nothing less
 
Utakuwa mgeni sana - tafuta zingine Msakila Kabende, Mkafrend utagundua kwamba kabla hujamaliza sekondari nilikuwa humu

Aidha, wote hatutakuwa na fikra zinazofanana kwenye issue kama za uchaguzi

Kama una hizo I'd zote, hii ni ya nini?
 
Kama unaakili ya kukaa usibiri ajira ya kuletewa kwenu,basi kaa uzekee hapo ulipo.
serikali ina wajibu wa kutengeneza mazingira bora ya vijana kujiajiri na kuajiriwa,, Halijafanyika ilo... ni porojo tuu unaongea kwa sababu wewe ushaajiriwa hujui maumivu familia zetu wanapata
 
Vijana ni kundi kubwa, muhimu na linaloongoza kwa uwingi wa idadi kubwa ya watu hapa Tanzania na kwasasa inaarifiwa zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania wote ni vijana. Vijana ni kundi kubwa lenye watu wengi na lenye msingi mkubwa sana wa uchumi na maendeleo.

Ukimkomboa kijana, umelikomboa Taifa. Ukimuwezesha kijana umeliwezesha Taifa yaani kwa kifupi chochote chanya utakachofanya kwa kijana umekifanya kwa Taifa na unakuwa umelikomboa Taifa. Miaka mitano ya Rais Magufuli imeshuhudia kazi kubwa sana ya kulikomboa Taifa kupitia kuliwezesha kundi hili la vijana ili kwa uwingi wake mkubwa ndani ya nchi liendelee kuwa msingi wa uchumi na maendeleo ya Tanzania.

Ili kuliwezesha na kulikomboa kundi la vijana kwa minajiri ya kuweza kuchangia pakubwa kwenye maendeleo ya Taifa, Serikali ya Rais Magufuli iliweka sheria ya kuzitaka halmashauri zote nchini kutenga asilimia 4 kati ya 10 ya mapato yake ya ndani ya Serikali kwa ajili ya kwenda kwenye makundi ya vijana. Kutoa mikopo hii ya halmashauri isiyo na riba kwa makundi ya vijana ili kuanzisha biashara na kujiendeleza ni msingi wa kuwakomboa vijana na mpaka hapa tunapoongea jumla ya bilioni 28.2 zimeenda kwa vijana kutoka bilioni 2.3 pekee zilizopelekwa mwaka 2015.

Zaidi Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya vikundi mbalimbali vya vijana kupata mikopo kwenye mabenki yetu na taasisi za fedha kwa riba na masharti nafuu sana ambayo hayamkandamizi wala kumuumiza kijana na kumfanya asiendeleze biashara yake vizuri tofauti kabisa na ilivyokuwepo huko nyuma.

Lakini uamuzi wa kutoa vitambulisho vya mjasiriamali kwa elfu 20 tu ni ukombozi mwingine kwa vijana kwa sababu asilimia kubwa ya wajasiriamali hawa ni vijana. Hapo unazungumza kijana kutoka kufukuzwa, kubughudhiwa na kutozwa makodi kila siku mpaka kulipa elfu 20 tu na kuendesha biashara zake kwa mwaka mzima popote Tanzania.

Zamani mjasiriamali alikuwa na msululu wa makodi na kwa mwaka mmoja mjasiriamali alikuwa analipa laki 3 mpaka laki 5 na alikuwa anapata bughudha na kuonewa sana kwenye biashara yake, leo hakuna tena mambo hayo. Kitambulisho cha elfu 20 tu kinatosha kwa kijana kufanya shughuli zake kila mahali nchi nzima bila shida na bughudha yoyote kutoka kwa mtu yeyote ile.

Hapo hujaweka uamuzi wa Serikali kutoa mafunzo ya ujuzi katika stadi za kazi ambapo vijana 7,800 wa kada mbalimbali walipata mafunzo ikiwemo na wengine 52,353 waliopatiwa mafunzo mahali pa kazi na vijana 8,980 waliopatiwa mafunzo ya kilimo huku Serikali ikitengeneza ajira 6,032,299 katika sekta rasmi na zisizo rasmi ambazo nyingi ziliwagusa vijana.

Katika kuendelea kuliamsha na kulijumuisha kundi la vijana kwenye uchumi, Serikali ilitekeleza miradi mikubwa minne ya kimkakati ambayo iliwagusa vijana moja kwa moja kupata fursa za ajira na kutengeneza uchumi wao.

Hapa tunazungumzia mradi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) ambao pekee yake ulitoa jumla ya ajira 14,139 kwa vijana, mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal III) ambao ulitoa ajira 1,056, mradi wa Bwawa la kufua umeme wa Julius Nyerere ambao ulitoa ajira 3,412 pamoja na mradi wa Ubungo Interchange ambao nao ulitoa ajira 502 kwa vijana. Vijana hawa hawana cha kupoteza na hawa wana jambo lao la shukrani mapema kabisa siku ya Jumatano Oktoba 28.
umejitahidi kuelezea kwa urefu lakini ni sawa shati chafu unapulizia perfum!
 
Haishtui vijana wa baa za vichaa yani Bavicha, sera zenu na mgombea wenu ni matusi tu. Dawa yenu ni moja tu kura ya ndio kwa Magufuli.
Hakuna kura ya ndiyo kwa mgombea yeyote. Iliondolewa mwaka 1992. Jielimishe hilo ili upige kura kwa unayemtaka
 
Huu ni uchafu kama uchafu mwingine.
 
Vya kufokeana na kupangiwa wa kuchagua
Sisi waTanzania hatuviwezi kakweli, vyaivyo vya nini Sasa vya kufokeana.

Najaribu tu kukumbuka kwa sauti ya kule Kagera.

Ila atakae mpigia kura Yule jamaa mnyenyekevu wa kwenye mabango akapimwe anaweza kua na tatizo la usugu wa matatizo.

#Niyeye
 
Screenshot_20201016-161954.png
Screenshot_20201016-161713.png
Screenshot_20201016-161641.png
Screenshot_20201016-161606.png
Screenshot_20201016-132803.png
Screenshot_20201016-132715.png
Screenshot_20201016-061345.png
Screenshot_20201016-060258.png
Screenshot_20201016-060238.png
Screenshot_20201016-060153.png
Screenshot_20201016-055847.png
 
Back
Top Bottom