Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
ACHENI KUBETI.
1)Soka limekuwa shoka,vijana linawakata.
Mifukoni wachongoka,pochi zabaki ukata.
Mipesa inatoweka,shilingi wanazopata.
Vijana nawausia,sasa acheni kubeti.
2)Akili zawaponyoka,kamari kawakamata.
Umasikini wafika,beti hilo la utata.
Kazi zinasahulika,kubeti mnaitaka.
Vijana nawausia,sasa acheni kubeti
3)akili zinabenuka,kama ndoo bila kata.
Wilaya tunaśhituka,mkoa hadi na kata.
Vijana mnapetuka,na sheria mwazikata.
Vijana acheni nawausia,acheni sasa kubeti.
Shairi=ACHENI KUBETI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
1)Soka limekuwa shoka,vijana linawakata.
Mifukoni wachongoka,pochi zabaki ukata.
Mipesa inatoweka,shilingi wanazopata.
Vijana nawausia,sasa acheni kubeti.
2)Akili zawaponyoka,kamari kawakamata.
Umasikini wafika,beti hilo la utata.
Kazi zinasahulika,kubeti mnaitaka.
Vijana nawausia,sasa acheni kubeti
3)akili zinabenuka,kama ndoo bila kata.
Wilaya tunaśhituka,mkoa hadi na kata.
Vijana mnapetuka,na sheria mwazikata.
Vijana acheni nawausia,acheni sasa kubeti.
Shairi=ACHENI KUBETI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com