Vigogo Uhamiaji wana utajiri wa kutisha

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
0001kikwete.jpg

TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA

Mwandishi Wetu(GAZETI MWANANCHI)
KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.

Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.
Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.
Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.
Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.
Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.
Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.
Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.
Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.
Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa ‘kufanya kufuru' ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.
Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.
"Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali," imedai.
Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao."
Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.
Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.
Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.
Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.
Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

"Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo," alisema.

Wahamiaji haramu
Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.

Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.

Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo.
 
Wala hainishangazi maana siku hizi mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake.Haiwezekani kila wakati wasomali wawe wanakatwa kule kusini wakati entry point ziko kaskazini. Lazima iwe biashara ya watu wajanja ndani ya system zetu
 
ni kweli kabisa, mm hapa kazin kwetu ni ofisi ambayo tupo wafanyakazi kama watu 100s kati ya hao 70 ni wahindi 5 wakenya, kila mara jamaa wa uhamiaji huja na kupewa chochote kitu na kuwapa vibali feki na kuwapa mbinu jamaaa(indians) tena huwez amini anaewaunganisha ofis na uhamiaji ni kahindi kamoja kana kaa pale mtaa wa olimpio Upanga opposite na makaburi ya kisutu

na mwengine jamaa wa uhamiaji anajenga nyumba pale maeneo ya kndon wachina ndio wanamjengea. jamani huyu jamaa ... ni kweli mshahara wake unaweza kuwaweka wachina kumjengea? ni rushwa tu za hawa jamaa na ndio zinatupelekea leo kuwaona viongoz wetu hawafanyi kazi kumbe hawa jamaa wa chini ndio wanaharibia
 
hata mimi natamani kupata kazi uhamiaji
kwani ndo kwenye maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Kuhusu wageni kufanya kazi nchini inakuwa ngumu kwa sisi wazawa kuweza kuwasaidia jeshi la polis kwa kuwa ukiwasaidia baada ya muda mfupi yule jamaa anahonga pesa nyingi mapolis na anaachiwa sasa inkuwa kazi kwako wewe au ninyi mliomchomea mnapigwa chini kazi kama unavyojua PRIVATE SECTOR NDIO WAMEJAA SANA,pa kulalamika huna,unakuwa kijiweni huna kazi familia ndio hivyo tena?watoto shule basi yaani shida tupu,sasa kwa mwanachi wa kawaida ambaye anategemea kazi kwa kila kitu na hana plan B ni ngumu sana KUTOA TAARIFA ndio maana wageni tunafanya nao kazi na sisi tunaona bola liende na watu wachache kama hao wanakuwa na UTAJIRI WA KUTISHA.
 
Hawa wageni wanatubana sana wazawa hasa ktk sekta binafsi ni wengi sana na hawana work permit na wachache wanatumia za field ambazo huziaupdate kila baada ya muda.
 
Monday, 21 May 2012 07:57
TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA

Mwandishi Wetu

KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.
Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.
Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.
Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.
Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.
Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.
Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.
Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.
Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.
Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa ‘kufanya kufuru’ ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.
Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.
“Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali,” imedai.
Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao.”
Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.
Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.
Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.
Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.
Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

“Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo,” alisema.

Wahamiaji haramu
Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.
Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.
Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo.

Tatizo la Tanzania siwo umaskini, ni uongozi wa Vigogo wa ccm kula kwa matonge mali za Taifa huku Watanzania walio wengi wakihaha kwa mlo wa siku na kukusa elimu na matibabu ya uhakika,Mungu ibariki Tanzania.

SITOKUBALI TENA UFIKAPO UCHAGUZI WA 2015 KUZA UTU WANGU KWA T-SHART NA KANGA ZA CCM.
 
jaman wahindi haramu wapo wengi, tena wengine hawajui kabisa kiswahili kama hauamini nenda upanga plot 85 kwa oil com, yaan hawajui kabisa kiswahili ni kihindi tu. na hawana uraia
 
TAKUKURU hakuna kitu hapo,wao wenyewe ni kati ya Taasisi zenye wafanyakazi wenye utajiri wa kutisha,kuwapa kesi kama hizo kupeleleza ni kuwatengenezea ulaji,kwanza wajisafishe wao kabla ya kwenda idara nyingine,sina imani kabisa na hao watu,kwanza wanavictimize watu wasio na uwezo wa kuwahonga,na mahakimu wa primary courst na mapolisi wa vyeo vya chini.Hao jama ni goood wastage of the meagre national resources.
 
godown, kwenye sonaras, bado makampuni, baadhi ya mabenki migodini, kwenye viwanda...kila muda fulani maafisa wa uhamiaji wanaenda kukinga...... halafu wasiwe matajiri?!!
 
Niliyasema haya katika moja ya makala yangu huko nyuma. Ni dhahiri kuwa uhamiaji kuna ubadhilifu sana na sijui kwa nini serikali ilikaa kimya miaka yote hii. Fika uhamiaji makao makuu, yaani pale ni kama sokoni tandale; watu wa kila aina aina mainly wasomali, wahindi, na waarabu huingia pale na kwenda moja kwa moja kuwaona wahusika bila hata kukaa foleni. Utakuta mtu (mwarabu, muhindi, msomali) amepewa pasipoti kumi za wenzake ila kuongea kiswahili hata english hajuwi sasa unajiuliza kazipataje? Nimeshuhudia kwa macho yangu mtu (mwarabu) kaja pale uhamiaji na baasha limejaa lundo la pesa kampa dada wa uhamiaji pale first floor makao makuu. Yule dada alikuwa ananishugulikia mimi then mwarabu alipofika tu akaitwa na yule dada kisha mwarabu akampa yule dada kijifurishi then yule dada akafungua ile baasha kiaina kuangalia kunani mle ndani, baada ya kuona mzigo akachekelea na kuniambia nikakae nisubiri pasipoti yangu wakati hata hajaniuliza swali lolote. Kule Arusha, kuna wasomali kibao pale mjini na wengi wao wanajihusisha na ujambazi wengi wakitokea Kenya ila ni raia wa kisomali kwani hata kiswahili hawajuwi. Sasa jiulizeni, wako pale na wanaingia hapa nchini kwa misingi ipi? Namanga (mpakani mwa TZ na kenya) kuna ujambazi wa kutisha na wahalifu wakubwa ni wasomali na polisi wa pale wanajua hili lakini wala hawajihusishi mpaka wasikie mtu kachinjwa ndiyo wanaanza kusaka watu. Kilimanjaro pale ni sawa na Arusha kwani pia kuna wasomali wengi tu pale pamoja na wakenya waishio hapa nchini kimagendo. Kigoma, Mwanza, na Kagera kumejawa na wanyarwanda pamoja na warundi waishio humu nchini bila vibali maalum na wengi wao wakijihusisha na uhalifu hapa nchini. Hii nchi inakwenda pabaya sana, tusipoangalia tutasambaratika.
 
Back
Top Bottom