Vigogo SMZ wahaha kutetea nafasi zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo SMZ wahaha kutetea nafasi zao

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jul 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mawaziri na baadhi ya watendaji wakuu wa serikali ya Rais Amani Abeid Karume wamekumbwa na hofu kufuatia upinzani mkubwa unaowakabili katika kutetea nafasi za ujumbe wa Baraza la Wawakilishi. [/FONT]

  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hatua hiyo imebainika baada ya hatua ya kujaza na kurejesha fomu za kuwania ubunge na uwakilishi kukamilika na kuanza hatua ya kuwahoji wagombea ili kujua uwezo na mipango yaliyojiwekea iwapo watashinda katika nafasi hizo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hali ngumu kwa vigogo hao ilijitokeza wakati wa kuhojiwa na wajumbe ambapo masuali ya ahadi za kuwapatia vijana ajira na kukamilisha miradi ya kijamii ndiyo yaliyowapa wakati mgumu zaidi. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Huko jimbo la Bububu, Mwakilishi Khatib Suleiman ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira alibanwa na wajumbe aeleze idadi ya vijana aliosaidia ajira au vikundi vya miradi ya maendeleo alivyoanzisha jimboni hapo katika kipindi cha miaka mitano.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika jimbo la Mwanakwerekwe, Makame Vuai Issa amejitokeza kwa kishindo kutoa upinzani kwa Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye ndiye Mwakilishi wa jimbo hilo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Nahodha aliamua kuchukua tena fomu ya Uwakilishi wa jimbo hilo baada ya kuanguka katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM nafasi ambayo imekwenda kwa Dk. Ali Mohammed Shein.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wengine wenye hali mbaya ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzibar, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, ambaye anachuana na ofisa wa Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji Fadhil Omar katika jimbo la Dimani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mawasiliano na Uchukuzi), Machano Othman Said anachuana vikali na kada wa CCM katika jimbo lake na Chumbuni, Sharif Shashi na kada mwengine wa CCM kijana Abbas.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika jimbo la Jang’ombe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ), Suleiman Othman Nyanga, amebanwa vikali na Abdallah Diwani na Mwatum Sultan.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhan Saadat Haji anakabiliwa na ushindani mkali katika nafasi ya uwakilishi jimbo la Kikwajuni, ambapo anachuana vikali na Mahmoud Mohammed Mussa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kinyang’anyiro kikubwa kimejitokeza katika jimbo hilo nafasi ya Ubunge inayoshikiliwa na Parmuki Hogan Singh hasa baada ya kujitokeza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhna Ferouz kuchuana naye.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Nae Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Khataib Suleiman Bakar anachuana na wagombea kadhaa akiwemo mshindani wake mkubwa Amour Khatib Makame, ambapo katika jimbo la Dole Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Shawana Buheity Hassan anachuana vikali na kada wa CCM Omar Gulam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika jimbo la Mji Mkongwe Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Sultan Mohammed Mugheiry anachuana vikali na Simai Mohammed Said na Meya wa zamani Zanzibar, Ahmed Keis na Nassor Mugheiry.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kutokana na ushindani huo, baadhi ya mawaziri na watendaji hao wameamua kutochukua fomu za kutetea majimbo hayo, baadhi yao ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mahmoud Rhabit Kombo ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Mpendae na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Muungano, Omar Yussuf Mzee.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mchakato wa kuwahoji wagombea ulioanza juzi unaendelea katika majimbo mbalimbali, ambapo baadhi ya wagombea wamekuwa wakichukua tahadhari ya kupandwa na ugonjwa wa mshituko wa moyo na sukari na kulazimika kutembea na dawa za maradhi hayo.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE

  Kuna Kasheshe huko Visiwani,jamani Uongozi ni mtamu kazi ipo huko Visiwani.
   
Loading...