Vigogo CCM wapania 'kumnunia' Mwenyekiti

Vigogo CCM wapania 'kumnunia' Mwenyekiti

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Katika kile kinachoonekana kuwa marekebisho ya Baraza la Mawaziri yamepokelewa kwa maoni tofauti,vigogo wa ngazi za Taifa wa CCM jana walipania 'kumnunia' Mwenyekiti wa chama Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kile walichodai kuwa 'hakuwasikiliza'. Hatahivyo,Wajumbe hao hawakusema namna watakavyomnunia Mwenyekiti.

Taarifa kutoka ndani ya kikao kilichoitishwa na kuongozwa na Katibu Mkuu Kinana na kufanyika jana,zinasema kuwa ingawa suala la Baraza la Mawaziri halikuwa ajenda ya mkutano huo,mjadala mzito na wenye mvutano mkali juu ya suala hilo uligubika kikao hicho.Kikao kilipanga kutathmini na kupanga mipango juu ya hali ya Uchaguzi Mdogo katika Kata 27 unaofanyika Februari.

'Yaani Katibu Mkuu alilazimika kuizima hoja hiyo kwa kutumia mamlaka yake tu.Lakini hali ilikuwa tete.Wajumbe walichachamaa na kupania kumnunia Mwenyekiti. Walitaka asikilize chama juu ya Mawaziri waliopendekezwa kuachwa' kilisema chanzo hicho cha kuaminika toka kikaoni.

'Ilifikia wakati wajumbe walikuwa wanataja Mawaziri waziwazi huku wakiwaita 'hawafai' na juhudi za kuwanyamazisha mwanzoni zilielekea kugonga mwamba. Ndipo Katibu Mkuu alipotumia mamlaka yake kichama kwa kutoa na mikwara kuhusu mipaka ya chama kwa Rais. Hali ni tete chamani.' aliongeza Mjumbe huyo wa mkutano huo.

Nisingekuwa na udhuru jana,ningekuwepo kikaoni.Nimekosa uhondo wa moja kwa moja. Lakini,chanzo changu nakiamini na kukikubali. Kwakuwa CCM ni chama imara,kila kitu kitakwenda sawa. Hatahivyo,umakini wa uongozi wa juu unahitajika sana wakati kama huu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

 
Kinana sasa asuke ama kunyoa,ujangili wake utaanikwa na wahafidhina.
 
itafika mahara watanzania wote tutazungumza lugha moja! na kuukataa uongozi dharimu wa chama cha magamba(CCM) waz waz bila kujali itikadi zetu" naliona anguko la ccm uchaguzi wa 2015
 
Nape kijana wangu chukua maamuzi magumu mmepuuzwa vyakutosha.
 
Wenye akili wamegundua tayari kuwa ccm imekata ringi kitaa,hivyo uhakika ni kuwa anayeamini ccm ipo imara bila shaka anapaswa kuchunguzwa akili zake haraka sana kabla ajaanza kuwadhuru raia mtaani au kutembea mtupu. Ahsante MUNGU kwa kifo cha CCM maana nina imani mapema 2016 nchi mikononi mwa CDM tutaanza kushuhudia mabadiliko chanya katka kila sekta.
 
Naomba kuuliza, hivi mawaziri wanachaguliwa na chama au ni Rais ndo kapewa majukumu hayo na katiba? Maana naona kuna watu wanadhani kuwa members wa chama wanadhani wana mandate ya kuamua nani atoke kwenye baraza na nani achukue nafasi gani. Kwa wenye uelewa zaidi wa vifungu vya sheria vinavyotoa mamlaka ya kuteua au kupiga chini mawaziri atusaidie

The Don
 
CCM vipande vipande
Mkuu Lwesye,CCM bado ni moja ingawa mitazamo si mimoja...ha ha ha ha

Naomba kuuliza, hivi mawaziri wanachaguliwa na chama au ni Rais ndo kapewa majukumu hayo na katiba? Maana naona kuna watu wanadhani kuwa members wa chama wanadhani wana mandate ya kuamua nani atoke kwenye baraza na nani achukue nafasi gani. Kwa wenye uelewa zaidi wa vifungu vya sheria vinavyotoa mamlaka ya kuteua au kupiga chini mawaziri atusaidie

The Don
Mkuu,chini ya Ibara ya 55(1) na (2) mwenye Mamlaka ya kuteua Mawaziri na Manaibu ni Rais wa Jamhuri tu baada ya kushauriana na Waziri Mkuu

Nape kijana wangu chukua maamuzi magumu mmepuuzwa vyakutosha.
Maamuzi gani Mkuu WILLAFRICA?

hakuna mwenye ubavu huo
Wakiwepo je? Subiri uone

Angaikeni tuu ccm siyo chadema eti
Unamjibu nani kijana? Umenikuta na utaniacha CCM

Mzee Tupatupa wa Lumumba
 
Last edited by a moderator:
Wengine humu jf ni vikaragosi ht kadi kupigia kura hawana halafu Maneno mengii
 
Kikwete komaaa baba,usipelekeshwe na mtu,wewe ndio na rais na mwenyekiti wa chama tawala.
Kwani wakinuna si wanajinukisha vinywa vyao wenyewe?
 
Watanzania wana imani na ccm,chadema wana imani na mbowe au slaa,cuf wana imani na lipumba au maalim seif sharif hamad,ccm ni taasisi imara ya kisiasa ,vyama vyenu ni taasisi bomu,zinazoongozwa na waigizaji imara.ccm,ccm,ccm !!!
 
Nilishamdharau Nape baada ya kusema kuna mawaziri mizigo, alikosa njia sahihi ya kufikisha ujumbe wake kwa rais kikwete??
 
Kikwete komaaa baba,usipelekeshwe na mtu,wewe ndio na rais na mwenyekiti wa chama tawala.
Kwani wakinuna si wanajinukisha vinywa vyao wenyewe?
 
Back
Top Bottom