Vigogo CCM 'wahamia' Marekani

Vigogo CCM 'wahamia' Marekani

mgomba101

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2011
Posts
1,822
Reaction score
711
VIGOGO watano wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wako nchini Marekani, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Uwepo wa vigogo hao Marekani kwa wakati mmoja, umeibua gumzo nchini hususan kwa mitandao ya makada wa chama hicho wanaotajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015.

Vigogo hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), Abdulhaman Kinana, ambaye amepata kuwa kampeni meneja wa marais hao wawili.

Mwingine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa makada watakaowania urais mwaka 2015.

Wakati vigogo hao wako nchini Marekani, kigogo mwingine wa CCM, Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, anatarajia kwenda nchini Marekani kesho.

Ingawa vigogo hao wako Marekani kwa shughuli na sababu tofauti, mahasimu wa Waziri Membe kisiasa wamehusisha ziara hiyo ya wazito hao na harakati za urais 2015.

Rais Kikwete yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. Rais na ujumbe wake uliondoka nchini juzi na atakuwa hapo kwa siku mbili kabla ya kuelekea nchini Canada kwa ziara nyingine rasmi ya kiserikali.

Habari zinasema kuwa Mkapa na Kinana waliondoka nchini wakati vikao vya mchujo vya CCM vikiendelea mjini Dodoma na wako nchini humo kwa ajili ya shughuli za taasisi ya Mkapa Foundation na Nape anatarajia kwenda kwa shughuli zake binafsi.

Hadi sasa hakuna kada yeyote wa CCM aliyetangaza kuwania urais, lakini mbali ya Membe, duru za kisiasa zinawataja makada wengine wanaotaka urais kuwa ni pamoja na mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Hata hivyo, kasi ya Sumaye kuwania nafasi hiyo imepunguzwa na matokeo ya uchaguzi wa NEC, wilayani Hanang' ambapo aliangushwa na Dk. Mary Nagu.

Wengine ni Samuel Sitta, Dk. Abdallah Kigoda, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha Rose Migiro na wengine.

Source: Tanzania Daima
 
Wemeenda kumsimika Membe kwa chifu wao Obama kama raisi ajaye wa Tz na yeye aanza kuwekewa uswiss 10 % za gesi kwa ajili ya kampeni za uchaguzi ujao.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wameenda kutengeneza mazingira kabisa maana kikinuka 2015, wapate pa kwenda kukaa.
Maana washasoma upepo bahada ya matokeo ya NEC, kwani wao akishinda Lowassa watafia lupango, na M4C ikiingia madarakani ndio kabisa. labda Rose Migiro.
 
Hiyo ni kambi ya JK kuelekea urais 2015, wameicha kambi ya Lowassa na Sita shambani kwa bibi
 
Du afadhali hukunitaja, na mimi, niko kwenye msafara huu, ila mimi nitaelekea canada moja kwa moja kwaajili ya maswala ya kiusalama. Dont ask mimi ni nani, i wont tell u.
 
Du afadhali hukunitaja, na mimi, niko kwenye msafara huu, ila mimi nitaelekea canada moja kwa moja kwaajili ya maswala ya kiusalama. Dont ask mimi ni nani, i wont tell u.

mwisho wenu 2015
 
wameenda kumuangukia BUSH, na kumuambia issue ya kigamboni imestukiwa,
ok watakuwa wameenda kusaini mkataba wa Gasi na Uranium.
 
Bora tu wahame kwa hiyari kabla hawajahamishwa 2015!!!!!!!!
 
Pesa za GAS; Halafu NAPE NNAUYE atuambie hakuna UFISADI!!!
 
Yuu! una maana wanajidai kumsahau Lowasa? Ni lazima wampe huo uraisi kwani naye anauhitaji sana. Huko kwa Bush kutachacha tu kwani Obama alishamshtukia. Rais wa wapi kila siku hodi? Yaani maandazi, vitumbua, kuku, mbuzi, mbwa, Ako! Obama alishachoka hata kusikia hilo jina.
2015 ndiyo tu mwaka utakaoirudishia Tanzania heshima yake.
 
Kila kiongozi yupo ughaibuni.. Kwa taarifa nlzozipata hatya makinda,pinda na bilal nao wapo nje duuuh hii balaa naona meck na sadick na mama salma ndio wameachiwa
 
Rais mstaafu Mkapa anatarajiwa kufungua jina jipya la DCB commercial bank leo pale Magomeni. Hajarudi?
 
Back
Top Bottom