Vigogo Benki ya Ushirika K'njaro wafutwa kazi kwa ufisadi

fred mwakitundu

Senior Member
Joined
Dec 31, 2018
Messages
123
Points
250

fred mwakitundu

Senior Member
Joined Dec 31, 2018
123 250
Maofisa watano wa Benki ya Ushirika Mkoani Kilimanjaro(KCBL)wamefukuzwa kazi kutokana na tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za benki hiyo.

Waliofukuzwa kazi ni pamoja na aliyekuwa meneja Mkuu wa benki hiyo,Joseph Solomon Kingazi,Ombeni Andrea Masaidi,Asha Hamis Kisega,Ukundi Leornard Mmochi na Doe Fidelis Mashinga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya uongozi wa benki hiyo,maofisa hao wamefutwa kazi kuanzia April 29 mwaka huu na benki hiyo imetoa angalizo kwa wateja wake pamoja na wananchi kuwa haitahusika na taarifa au miamala yeyote itakayofanywa na watu hao.

Kufukuzwa kazi kwa maofisa hao kunatokana na benki hiyo kuyumba kuichumi ktokana na ufisadi mkubwa uliokuwa ukifanywa na maofisa hao hasa kwenye eneo la mikopo ambako benki hiyo imeshidwa kurejesha mabilioni ya fedha yaliyotolewa kwa wateja mpaka sasa.

Kutokana na kuyumba kwa benki hiyo,benki kuu iliiweka kwenye orodha ya benki zilizostahili kufutwa kutokana na kushindwa kumudu masharti ya benki kuu ya kuwa na mtaji wa kiasi cha Bilioni tano amako mtaji wa benki hiyo mpaka sasa upo chini ya sh,Bilioni mbili.

Mpaka sasa benki hiyo imeshindwa kuendelea na utoaji wa huduma za kibenki na wateja wa benki hiyo hawaruhusiwi kutoa fedha zao na wamelazimishwa kuzibadili amana zao kuwa hisa .
 

Forum statistics

Threads 1,382,570
Members 526,405
Posts 33,831,636
Top