Vigezo vya kuupata uprofessor nchini vimulikwe

Vigezo vya kuupata uprofessor nchini vimulikwe

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,363
Reaction score
17,597
Jamii inatumia kodi zao kuwasomesha wanataaluma wao ndani na nje ya nchi lakini kinachorudi kwao kutoka kwa wanataaluma wao hakilingani na thamani ya kodi zao.
Wasomi nguli wamejichimbia sehemu zisizofikika kwa urahisi na wanajamii wengi wa kawaida kupata huduma. Wasomi walio wengi nchini wanapanda vyeo na ngazi hadi kuupata uprofessor kwa kusoma kusoma kusoma na kufanya tafiti tafiti tafiti ambazo nyingi ya hizi tafiti zinaishia kwenye makabati yao, na kibaya zaidi haziwafikii wananchi waliowengi kwakuwa zimefungiwa kwenye masanduki yenye lakiri za lugha za kigeni. wananchi wengi wa kawaida wanashindwa kuzisoma kwakuwa zimeandika kwa kiingereza.

Badala ya uprofessor kupatikana kwa kufanya tafiti nyingi alizofanya mtu ni vema upatikane kwa namna msomi huyo alivyoihudumia jamii yake iliyomzunguuka kwa miradi inayoguza maisha ya watu wa kawaida moja kwa moja kama vile kugungua, kubuni, kuhudumia na kuandika vitabu vitakavyosaidia jamii na kubakia kwenye jamii hata wao watakapokuwa hawapo kwenye kutoa huduma. Kufanya tafiti ni sawa lakini tafiti pekee zinazoishia kwenye mashelfu ya kwenye Idara yasitoshe kwa mtu kupewa uprofessor.

Mfano, mtu anaweza kuwa ni Professor wa Nutrition lakini jamii haina habari kuwa madini ya folic acid yanatosha kuzuia watoto kuzaliwa wakiwa na shida ya mgongowazi, vichwa vikubwa au midomosungura. Hakuna kampeni, kitabu wala jarida la kiswahili linalozunguuka kwenye jamii kuhusu manufaa ya folic acid. Mtu kama huyo atawezaje kuitwa Professor wa Nutrition? Hivyo hivyo kwa malaria, kisukari, cholera, n.k.

Shule na vyuo vinaagiza vitabu kutoka Ulaya na Marekani ili kufundishia wanafunzi wao Malaria na Cholera lakini kuna maprofessor hapa nchini hii ni sawa? Maprofessor ma- engineer wa ujenzi wapo lakini daraja linajengwa na engineer kutoka China hii nayo ni sawa? hata kama hana vifaa na mtaji lakini hata kuandika vitabu ili visomwe na watengeneza matofali na wapiga plasta wadogo kabisa nayo ni kazi kubwa hiyo? wanakuwa maprofessor kivipi hawa? Wizi mtupu!!! Mbao za magazeti zimejaa vijitabu na magazeti ya hadithi na mapenzi vilivyoandikwa na watu wa kawaida kabisa lakini vitabu vinavyoelezea ufugaji wa kuku, kilimo cha alizeti au namna ya kujikinga na malaria havipo.

Ni heri msomi mmoja aliyeandika kitabu kimoja chenye manufaa kwa wananchi wengi nchini kupewa uprofessor kuliko aliyeandika paper 1000 zilizohifadhiwa kwenye kabati lake. Mtu kama Prof. Ndalichako unaona kabisa kuwa alistahili kuitwa Professor, unaona jinsi anavyothubutu na kuhangaika na elimu ili ikae sawa na kuinufaisha jamii. Yuko Prof. ambaye jamii inashindwa kufahamu ni professor kivipi, akifa basi na uprofessor wake umekufa imekwisha hana alama labda ya wanafunzi wake aliofundisha ambao nao watazeeka na kufa, hakuna kitabu, hakuna sindano aliyotengeneza wala kifungo cha shati.

TCU pita vyuoni ili uone maprofessor wako wanaisaidiaje jamii hii ya watanzania badala ya kudai tu kuonyeshwa research ngapi mtu kafanya. Maprofessor hawa wangelisaidia taifa kuepuka gharama za kuagiza vitabu nje ya nchi vya kufundishia shuleni vitu ambavyo viko zaidi hapa Tanzania kuliko Marekani au ulaya, vyuo vya ufundi kama veta wanahitaji vitabu, wananchi wa kawaida wanahitaji vitabu kwa lugha yao lakini havipo kwenye jamii. TCU isaidieni Tanzania kwa kuwalazimisha wanataaluma kuihudumia jamii kuliko kurundika vyeti na research papers kwenye Idara za vyuo. Vitu hivi viende sambamba
 
ELIMU yetu ni Pesa, ukiwa na Pesa chukua Masters ya kununua, kisha PhD ya kununua. U Profesa NDIYO simpo. Cha msingi kusanya vijipesa
 
Back
Top Bottom