Vigezo vipi vinatumika mwajiri kukuchukua

Vigezo vipi vinatumika mwajiri kukuchukua

matunge88

Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
58
Reaction score
26
Habari wana JF.

Napenda kujua vigezo vipi vinatumika wewe/mimi kuchaguliwa kati ya wasailiwa wa nafasi ya kazi. Nimefanya interview kama mbili hivi naona kabisa nimefanya vizuri lakini nikakosa kazi, nilimpigia simu HR wa hiyo kampuni kumuuliza kigezo gani kimenifanya nikose hiyo kazi, akaniambie usaili nimefanya vizuri tu kwa 75% lakini kigezo cha pili cha uzoefu kazini ndo kilininyima kazi kulingana na kazi nilizoonyesha kwenye CV yangu.

Naamini humu JF kuna HR wengi tu na wamebobea sana kusaili watu, wanisaidie vikezo vipi vya msingi vinamfanya msailiwa apate au kukosa kazi kulingana na majibu ya huyo HR.

Nawakilisha.
 
kujuana kwa sana, hr depatment wengi wanaweka vimada wao,ndugu zao na marafiki zao
 
Wasingekuita kwenye usaili kama waliona hauna uzoefu wa kutosha,ila jua kwamba wewe unahisi ulifanya vizuri je unajua na wenzio mlioshindana nao kama hawakufanya vizuri?
 
Bias from interviwee ndo inazngua siku zote
 
kujuana kwa sana, hr depatment wengi wanaweka vimada wao,ndugu zao na marafiki zao

ndio mana yake hao wanaowaweka wengine hawana hata chembe ya uzoefu hapo walikutafutia sababu tu.
 
pengine kuna waliofanya vizuri zaid yako,tatizo umeassume wengine waliofanya intavyuu ni vilaza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom