Vifungashio vya plastiki mwisho Aprili 8

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
BAADA ya Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, sasa imechukua hatua zaidi kwa kutoa muda hadi Aprili 8, 2021 kuwa mwisho wa matumizi wa vifungashio vya plastiki vinavyotumika kufungashia bidhaa ndogo ndogo yakiwemo maji, karanga na ubuyu.

Akizungumza katikaa ziara ya Makamu wa Rais kwenye Uwanja wa Tangamano mkoani Tanga, Mbunge wa Tanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Ummy Mwalimu alisema mwisho wa matumizi ya vifungashio hivyo ni Aprili 8 ambapo baada ya hapo atakayebainika anatumia vifungashio vya plastiki atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kulipa faini Shilingi laki tano.

Kauli hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Samuel Gwamaka alipokaiririwa akisema kuwa wamebaini vifungashio hivyo vinazalishwa kwa wingi kwa ukubwa na vimekuwa vikitumika kama mifuko ya kubebea bidhaa sokoni.

Alisema katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wazalishaji wa vifungashio vya plastiki aina ya “tubings” vinavyotumika kufungashia bidhaa kama karanga, ubuyu na barafu, vikiwa havina kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na lakiri (seal) wala alama (label) kama kanuni namba tatu inavyoelekeza.
 
Duh....
Tanzania limegeuka kuwa Taifa la marufuku.

Siasa marufuku, upinzani ni marufuku, Mifuko marufuku, vifungashio marufuku, tuisheni marufuku, kuuliza Manunu Yuko wapi marufuku, kuhoji ni marufuku, kudai katiba mpya ni marufuku, kukosoa ni marufuku, kujitetea ni marufuku, kujihami ni marufuku.

Yaani ni mwendo wa.marufuku tu.
 
Busy na Mifuko ya plastic ambayo kimsingi mi sijaona inachafuaje Mazingira, Miti inakatwa kila siku na haipandwi mipya, watu wanasafisha misitu hekali na ma hekali kwa ajili ya kilomo hakuna hata tozo za uharibifu wa mazingira, watu wanakojoa wakiwa wanaogelea baharini hata halisemewi tupo busy na mifuko ha haaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom