Vifo vya viongozi vyenye utata

Kuna vifo vya mwenyezi Mungu na vifo vya kupangwa na watu
 
MH ila minajua mungu ndie mpanga urefu/ufupi wa maisha ya kiumbe hapa dunian
 
PRO.JWAN MWAIKUSA,MGIMWA,jaribio la kuwaua MWAKYEMBE NA MWANDOSYA
 
Wadau mtakumbuka kwamba huyu mheshimiwa Dr. Omar Ali Juma alikuwa makamu wa rais wa JMT na ghafla mwezi Julai mwaka 2001 wakati wa maadhimisho ya Sabasaba baada ya kutembelea maonesho hayo akionekana mwenye afya nzuri kabisa, alfajiri ya tarehe 5 Julai ndo tulitangaziwa kwamba alikuwa amefariki dunia kwa shinikizo la damu. Hata hivyo, baadae yalisemwa mengi kuhusu kilichosababisha shinikizo hilo la damu. Wengine wanadai kwamba aliauawa. Sasa nakuja kwenu wadau, hivi kifo hiki kilisababishwa na nini hasa? Karibuni tufunguke kila mtu kile anachokijua kabla sheria yao haijaanza kutumika. Nawasilisha.
 
Umetumwa na nani? Tuambie wanaosema aliuawa! Na wanatoa sababu zipi? Mgimwa mdogo alisemaje bungeni kuhusu kifo cha baba yake?
Tuko kwenye harakati za uchaguzi usiturudishe nyuma!
 
Inasemekana ni kasumu flani ivi aliekewa kwenye microphone ama katika kajuice ivi aliyokunywa wkt wa chakula alipotoka kwenye hayo maadhmish
 
Wauaji ndo hawa tunaoendelea kuwapa ridhaa na lichama lao
 
Kuna maneno mengi kuhusiana na kifo cha Dr Omary sababu kubwa zaidi yaweza kuwa uRais awamu ya nne.

Kuna mwanajamvi mmoja ni mahiri sana katika haya masuala bahati mbaya nimesahau jina.
 
Inasemekana alifokewa na Che Nkapa moyo ukamwenda mbio mithiri ya mtoka nduki usain bolt na hatimae israel akabisha hodi akatuachia mwili tu roho ya mpendwa wetu Dr Ommy alitokomeanayo kusikojulikana.
 
muanzisha mada yaelekea unajua vizuri na mengi kuliko wachangiaji wote..
 
Wee mleta mada umetumwa na nani wewe kukumbusha yaliyopita?au na wewe ulikuwa miongoni mwa Wahanga wa ''Mtandao'' uliokuwa chini ya Mamvi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…