Vifo vya malaria vyapungua duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo vya malaria vyapungua duniani

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 27, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Imetafsiriwa na Zawadi Machibya
  [​IMG]Mamilioni ya vyandarua vimesambazwa kudhibiti malaria Afrika


  Wote tunapenda ripoti za kitabibu zenye mafanikio makubwa ya kisayansi lakini ukweli ni kwamba maendeleo ni ya hatua kwa hatua na mambo muhimu mengi yanaweza kuachwa.

  Chukua Malaria. Vifo vinavyotokana na maambukizo ya vimelea na kusambazwa kwa kuumwa na mbu vimeanza kupungua tangu mwaka 2004. Miaka michache tu iliyopita iliarifiwa kuwa ugonjwa huo ulikuwa unaua mtoto mmoja kila baada ya sekunde 30. Mpaka mwaka 2009 makadario yalikuwa chini mtoto mmoja alikua akifa kwa kila sekunde 45.
  "Sasa inaelekea kuwa malaria inaua mtoto kila baada ya sekunde sitini." Kwa mujibu wa Dr Richard Cibulskis, Muandaaji kiongozi wa Ripoti ya Malaria Duniani.
  Alifafanua kuwa kuna vipengele vya kitakwimu vinafanya kazi hapa, kwa sehemu kupungua kwa vifo kunatokana na kurejewa kwa mapitio kuhusu vifo vya watoto duniani kwa ujumla wake.
  Mapitio mapya katika miaka ya karibuni yamesababisha kupungua kwa makadirio ya matukio.
  Kutathmini uzito wa malaria si kitu cha moja kwa moja. Nchi nyingi za Afrika hazina mfumo madhubuti wa magonjwa kuweza kutunza takwimu za vyanzo vya vifo si mara zote vinarekodiwa vyema. Hii ina maana kuwa utafiti na kile kinachoitwa ‘uchunguzi wa maneno' wenye maelezo ya dalili za ugonjwa zilizoelezwa na wazazi mara nyingine ndizo zinazotumika.
  Kupiga hatua

  Licha ya ugumu katika kukusanya takwimu, iko wazi, kupungua kwa vifo hatua kwa hatua kunakaribishwa. Inakadiriwa kuwa malaria iliua watu 655,000 mwaka 2010, ikilinganishwa na vifo 800,000 mwaka 2004.

  "Ni hatua kubwa sana," alisema Dr Cibulskis.
  Kupiga hatua huko kunatokana na mambo kadhaa. Jumla ya vyandarua 145 milioni vilivyowekwa dawa ya muda mrefu vilisambazwa mwaka jana kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara, ongezeko kubwa kwa mwaka 2009. Kunyunyizia dawa kuta ni njia nyingine ya kupunguza malaria.
  Mtu anapoambukizwa tu ni vizuri aanze matibabu mapema. Vipimo vya mapema vinatumika kwa wingi sasa. Hii inaonyesha kuwepo kwa vimelea kwenye damu mara nyingi kwa kipimo cha kutoa damu kwenye kidole.
  Matumizi ya dawa ya artemisinin-iliyochanganywa na dawa nyingine yamefanya mabadiliko makubwa ya kutibu ugonjwa huo katika muongo uliopita.
  Watoto wanaoumwa sana wanaweza kupata matibabu na kupona haraka baada ya siku kadhaa za kutumia dawa hiyo.
  Usugu wa dawa

  Kuna dalili na wasiwasi wa usugu wa dawa, kwanza umethibitishwa katika mpaka wa Cambodia na Thailand mwaka 2009 na sasa unadhaniwa kuwepo Burma na Vietnam.
  Kupunguza kutokea kwa usugu wa dawa kuenea ni muhimu dawa ya mseto ya artemisininkutumika, bado nchi 25 nyingi zikiwa Afrika zinaruhusu kuuzwa kwa dawa ambazo hazijakamilika. Shirika la Afya WHO linasema watengeneza wakubwa ni India.
  Kuna ishara zinazoonyesha matumaini kutokana na majaribio ya chanjo dhidi ya malaria, lakini hiyo itakuwa ni sehemu tu ya suluhisho la kupambana na maambukizo yanayoweza kudhibitiwa.
  Kuna wasiwasi kuhusu mfuko wa fedha duniani (global fund) unaofadhili miradi ya kudhibiti malaria ambao unatarajiwa kufikia $2bilioni mwaka huu na kushuka hadi $1.5bilioni mwaka 2015.
  Serikali ya Uingereza ni mmojawapo wa wafadhili wakubwa na inaahidi kuongeza kwa miaka ijayo.
  Malaria inabakia kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma. Vifo tisa kati ya kumi vinatokea barani Afrika na wengi kati hao ni watoto chini ya miaka mitano.
  [​IMG]Anopheles, mbu anayeambukiza vimelea vya malaria


  Imeandikwa na Fergus Walsh Chanzo.
  BBC Swahili - Habari - Vifo vya malaria vyapungua duniani

   
Loading...