nandembako
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 655
- 525
Leo nilipata muda wa kupumzisha mwili mahali fulani...lakini bahati mbaya mara zote sijawahi kufanikiwa kupumzisha akili....wakati nikiwa naangaza huku na huku kabla ya kupitiwa usingizi,niligundua nimezungukwa na artficial environment vitu natural vilikuwa vyakutafuta sana,swali lilikuja kichwani na kujiuliza hivi haya mazingira yaliyowekwa na binadamu yanatusaidia nini katika kuishi...kwa kina nikifikiri kipi kinatusaidia kiafya,kuanzia majengo hadi vyakula....nikikumbuka zamani vitambi vilikuwa vichache sana,visukari vya kutafuta tuliita donda ndugu wengine mahali fulani hatukuwahi kusikia kabisa u.t.i kabisa...unene kupitiliza haukuwepo kama ilivyo leo,mtu akifa watu wanaagua hawaamini kama kifo kinaweza kusababishwa na magonjwa na vifo vilikuwa vichache....Sasa siku hizi mtu kufa kawaida sana,wanaoguswa moja kwa moja tu ndio wanabaki hawaamini kuwa ndugu yao ameondoka....
ANGALIZO:turudieni zama zetu,haya mambo mapya yanatumaliza....madawa tunayodhani yanatutibu yanatumaliza kabisa....vyakula ambavyo tunadhani ni lishe ni matatizo kwetu...inabidi utumie nguvu sana kuwa na afya yako ya kawaida...
HaTUROGWI TUNAJIROGA WENYEWE...
hawa WACHUNGAJI waende NIGERIA huko TANZANIA haturogani....