Umesema kilekile nilichofikiri.
Kuna watu wana uzalendo wa kizamani.
Mtu kauliza, that shows an inquisitive mind. Waswahili wamesema kuuliza si ujinga.
Hizi habari za kutaka "self censorship" kwenye kitu chochote kinachofanywa na jeshi kitafanya wajanja watumie jeshi na "usalama wa taifa" kufanya ufisadi wao wote.
Utafanya nini? Ukiulizwa utaambiwa "hilo ni suala la usalama wa taifa".
Utasema nini na wewe ushafanya jeshi na usalama wa taifa some "holy cow"?
Kama.jeshi limeamua kufanya gwaride lisilo rasmi, pengine thtead kama hii inalisaidia kuwapasha habari wananchi kwamba jeshi lipo, kwa nini mnataka kitu ambacho jeshi halijaficha kiwe siri hapa JF, ambapo tunajivunia uhuru wa kujieleza?
Wanaotaka kujua nyendo za jeshi letu ambao inabidi tuwahofie ni wenye satellites zinazoweza kuona mwendo wa kifaru kutoka anga za juu. Jeshi linajua hilo, na kama lingetaka usiri lingesafirisha vifaru vyake kwanusiri zaidi
Hawa watu wanaotaka self censorship inabidi wasome motto ya JF.
Jamiiforums. Where We Dare To Talk Openly.