Hujui thamani yake ndio maana unaongea pumba..ndio maana kuna mbuzi na kuku. Kwanini unanunua Bata Bukini laki 3 paka laki 4 kwa pear? Na Bata maji ni 40,000 kwa pear?
Nadhani jina - kuchi linachanganya pia. Nadhani hawa kuchi ni wa kigeni (exotic), kama ni hivyo ilipaswa wataalamu wetu kutohoa jina linaloonyesha ni aina ya kuku ambayo pamoja na kuwa na baadhi ya sifa zinazofanana na kuchi wetu (indigenous kuchi) lakini zina sifa za ziada, otherwise kuchi tunaowafahamu kijijini kwetu bei yao haiwezi kufika hata nusu ya bei unayotutangazia. Una nina nzuri ya kutangaza biashara, kinachokosekana kwenye tangazo lako ni kumfahamisha customer wako sifa za bidhaa yako. Otherwise wengine tutadhani labda kwa vile uko Arusha huenda watalii hununua kwa bei hiyo kuchi tunaowafahamu sasa unataka hata kina-sisi tununue kwa bei hiyo. Waelimishe watu tafadhali.