Vifaa vya umeme (Wiring materials) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifaa vya umeme (Wiring materials)

Discussion in 'Matangazo madogo' started by rmashauri, Oct 21, 2011.

 1. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wakuu ni duka gani kwa Dar es Salaam wanauza genuine (made in Europe if possible) wiring materials na vikorombwezo vyake kama vile soketi, swichi n.k. Niko kwenye hatua ya kufanya wiring kwenye nyumba mpya.
  Natanguliza shukrani zangu.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mkuu nami nipo hatua hiyo ila dar(kariakoo) naiogopa mbaya kwa vtu fake i was even thinking kwenda Kampala besides nasikia kule bei nzuri sana na quality unapakia ndani ya kampala coach hamna longolongo ya ushuru wala nn boda,ama nairobi,wadau acha watujuze kama iko duka ya uhakika twende tusipeleke pesa nje
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu yaani Kariakooo haiaminiki kabisa mpaka uwe unafahamu ni duka gani hasa waweza kupata vitu genuine. Na kama unavyojua umeme ni suala nyeti sana katika nyumba maana ukiwekewa vifaa feki ni hatari sana kwa maisha yenu na usalama wa nyumba yenu pia. Ngoja tusubiri wazoefu wa maduka Dar waje watuelekeze wapi ywaweza kupata vifaa genuine kwa ajili ya wiring.
   
 4. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Contact 0786148148 they have good quality staff not from Uk but of high quality wapo kkoo msimbazi stendi ya mbagala.
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante rafiki kwa kontakti za wauzaji wa vifaa vya umeme nitawatwangia
   
 6. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wakuu nadhani tatizo lililopo ni sisi wajenzi kwa kuwa tuko busy basi huwa tunawaamini mafundi wakatunulie vifaa. Nakwambia mafundi wengi lazima atakuchakachua na hata ukiongozana nae atakuwa amekwisha kwenda kuongea na wenye maduka ili wale chao cha juu. Na mbaya zaidi wakati mwingine ukienda wewe mafundi anakwambia ohooo mimi sikutaka kifaa hiki. Ukweli ni kuwa mafundi wengi wana njaa kali na ndo chanzo cha wateja wengi kulia. Am sure kuna product nzuri tu Kariakoo na ambazo nina uhakika nazo especially on that shop.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mkuu waashi ni kama mafundi gari, peleka gari,kuwa nae beneti anafungua anasema kibovu nawe japo unatumia knowledge kidogo kiangalie,mguu kwa mguu mnaenda shop mnanunua. Halikadhalika waashi,hata siku moja eti asikuwekee bill mezani unazama kwa wallet anaenda kununua,vifaa tafuta mwenyewe!muwekee pale afunge! wapiga panga sana jamaa kama viongozi wa ccm kwenye mikataba mbalimbali ya kitaifa!
   
 8. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 453
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Contact 0714779110.tuna kampuni inayojihusisha na electrical instillation,tuna maduka yetu yenye vifaa vya kuaminika kama vile switch,circuit braker,taa za aina mbalimbali,na tunatoa huduma za za ukarabati na service za umeme kwenye majengo mbalimbali hapa dar.
   
 9. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu kwa kontakti ina nina swali, products zenu mna import kutoka nchi gani?
   
 10. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 453
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sisi hatuimport ila kuna maduka ambayo tunanunua materials zenye uhakika kwa ajili ya tenda zetu tunazopata,hivyo katika kila kazi tunahakikisha tunatumia materials zenye ubora wa hali ya juu kwa sababu nia yetu ni kuimarisha soko la huduma yetu kwa sababu wateja tuliowafanyia kazi zao wameendelea kutupa kazi za maana zaidi,ni inbox nikujulishe moja ya tenda tunayofanya sasa hivi
   
 11. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nenda kariakoo mtaani wa Narung'ombe duka la Tropical wana vifaa vya ukweli, ushauri bure na guarantee ya kutosha. Nenda mwenyewe ukiweza kwani Mafundi lazima wale cha juu.
   
 12. kaygeezo

  kaygeezo Senior Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna hawa jamaa wapo morogoro road (just after ppf builiding) ukiifwata hiyo road ,wana vitu genuine na vya ukweli ,kuna mbabu wa kihindi pale atakupa ushauri
   
 13. N

  Ngo JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  rmashauri; Asante mkuu kwa kontakti ina nina swali, products zenu mna import kutoka nchi gani?

  [HR][/HR]
  Mkuu naona una wasiwasi na vitu toka China, siyo? Mpaka kiandikwe made in England/UK, Germany, Italy, nk ndo angalau uwe na imani na ubora wake. Kuna vitu vingi sana vinatengenezwa China bado vipo Imara, ukizingatia China inatumiwa na nchi nyingi zilizoendelea kama sehemu ya kuzalishia vitu kwa bei nafuu na kwenda kuviuza nchini mwao kwa bei kubwa. Zaidi ya asilimia 90% ya vitu vinavyouzwa US vimetengenezwa China na hayo makampuni ya US yaliyoamishia viwanda vyao China kuzalisha kwa gharama nafuu. Hivyo vitu vinavyozalishwa siyo vyote vinauzwa US, vingine vinaenda kwenye masoko mbalimbali duniani Ikiwemo Africa/Tanzania. Siyo kwa US tu wanaofanya hivyo bali kwa capitalist countries nyingi wanajaribu kupunguza gharama na kuongeza ushindani kwenye bei za kuuzia.[HR][/HR]
   
 14. N

  Ngo JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mihayo; Wakuu nadhani tatizo lililopo ni sisi wajenzi kwa kuwa tuko busy basi huwa tunawaamini mafundi wakatunulie vifaa. Nakwambia mafundi wengi lazima atakuchakachua na hata ukiongozana nae atakuwa amekwisha kwenda kuongea na wenye maduka ili wale chao cha juu. Na mbaya zaidi wakati mwingine ukienda wewe mafundi anakwambia ohooo mimi sikutaka kifaa hiki. Ukweli ni kuwa mafundi wengi wana njaa kali na ndo chanzo cha wateja wengi kulia. Am sure kuna product nzuri tu Kariakoo na ambazo nina uhakika nazo especially on that shop.[HR][/HR]
  Mihayo kama ulikuwepo vile maana hawa mafundi wetu ni hatari kweli. Kama mwezi umepita nilitaka kununua vitasa vya Milango, ikabini nimuulize fundi maduka gani naweza kupata vitasa vizuri vya milango. Jamaa akaniambia kuna maduka ambayo huwa ananunua vifaa vya ujenzi hapo Kariakoo vitu vyao vingi vina ubora siyo vya kuchakachua. Nikamwambia basi anichekishea kama wana design ya vitasa nilivyokuwa nataka na bei zao. Akaenda kuviangalia faster na kuja na bei. Tukakubaliana bei ya kuvifunga akawa amenitelemshia bei kido kulinganisha na mafundi wengine akijuwa ataenda kufidia kwenye manunuzi. Nilichokifanya siku ya kwenda kununua nikaenda nae, nikaviangalia na bei. Baadaye nikamwambia hapo bei zao ziko juu siwezi nunua, nikaenda maduka mengine niliyokuwa nayafahamu. Kitasa cha Tsh 110,000 kwa duka nililopelekwa na jamaa Tsh 130,000. Kwa idadi ya vitasa nilivyokuwa navitaka zaidi ya laki mbili jamaa angeondoka nayo. Hwa jamaa ni hatari, ni kujitahidi kwa kadili iwezekanavyo ila kubana angle zote si rahisi.
  [HR][/HR]
   
 15. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu upo TZ hii au uko nje ya nchi? Unachosema ni sawa kabisa, ila kumbuka kuwa kutokana na corrupt system yetu hapa TZ Wachina na wafanyabiashara wetu wanatuletea bidhaa za ubora wa hali ya chini sana kutoka huko China na India. Ulaya na Marekani wana sheria na wanazisimamia kwa uhakika kwahiyo wanapata bidhaa kutoka China zenye ubora wa hali ya juu. Kuna ushahidi wa zile bidhaa zinazoteketezwa kila mara hapa zikiwa hazina ubora vikiwemo vifaa vya umeme ambayo ni hatari sana kwa usalama wetu sote. So watchout mkuu.
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu. Hawa jamaa ndo wenyewe kwa hapa DAR wana vifaa vyenye quality ya juu na products zao ni make za Australia.
   
 17. THE RICHARDS

  THE RICHARDS JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2015
  Joined: Jun 18, 2014
  Messages: 2,711
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280

  wanauza mpaka vya jumla?
   
Loading...