Vifaa vya Uchaguzi vilikuwa vikitunzwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifaa vya Uchaguzi vilikuwa vikitunzwa na nani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gurtu, Nov 6, 2010.

 1. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pamoja na kuwa uchaguzi umeisha na uchakachuaji umeisha, mimi nina swali juu ya aliyekuwa anatunza vifaa vya uchaguzi kuanzia fomu, karatasi za kura na masanduku. Ninajua kuwa vifaa hivyo vilisafirishwa kutoka makao makuu ya tume hadi kwenye majimbo. Wakati wote huo na kupitia njia zote hizo usalama wa vitu hivyo ulikuwa chini ya nani?

  Tuseme kuwa vifaa vilikuwa vikisafirishwa na jeshi,polisi au usalama wa Taifa, je? hao walikuwa salama? Tunajua vilevile kuwa Tume haina waajiriwa katika ngazi zingine kama mikoa na Wilaya (au jimbo), hao watakao kuwa wanapewa vifaa hivyo wanawajibika kwa nani? Je, wakiamua kutumia vifaa hivyo kwa malengo yao au ya watu wao watawajibishwa na nani?

  Ni wazi kuwa Usalama wa taifa watakana kwamba wao hawahusiki na usalama wa vifaa vya uchaguzi na yote yanayoendana na uchaguzi, lakini tuambiane usalama wa vifaa vyetu ulikuwa chini ya nani?
   
Loading...