Vidonda mdomoni

Vidonda mdomoni

halloperidon

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Posts
2,101
Reaction score
5,266
Wakuu salaam,

Hili tatizo la kutoka vidonda mdomoni, lina miez sasa huwa natumiaga vitamin B12 huwa vinaondoka baada ya siku kadhaa vinarudi

Hasa vinatokea kwenye ulimi na lips, hadi kula nimekuwa mvivu jinsi vinavyouma, pia sometime vinaambatana na homa, fizi kutoa damu

Msaada wa mawazo dawa gani inaweza kumaliza hili tatizo ili niishi kwa amani naamini kuna madaktari humu

NB: mimi syo mpenzi wa kuzama chumvini na sijawahi

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
 
,

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu salaam,

Hili tatizo la kutoka vidonda mdomoni, lina miez sasa huwa natumiaga vitamin B12 huwa vinaondoka baada ya siku kadhaa vinarudi

Hasa vinatokea kwenye ulimi na lips, hadi kula nimekuwa mvivu jinsi vinavyouma, pia sometime vinaambatana na homa, fizi kutoa damu

Msaada wa mawazo dawa gani inaweza kumaliza hili tatizo ili niishi kwa amani naamini kuna madaktari humu

NB: mimi syo mpenzi wa kuzama chumvini na sijawahi

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app

KUTOKWA NA VIDONDA MDOMONI NA MATIBABU YAKE

Vidonda mdomoni husababisha sana maumivu makali pamoja na kumfanya mtu asiweze kuongea vizuri na watu.Vidonda hivi husababishwa na kutafuta kwa muda mrefu hasa bigijii au kitu chochote, uvutaji wa sigara,maambukizi ya virusi, bakteria na fungasi sambamba na ukosefu wa madini na virutubisho vya folic, zinc, vitamin c,vitamin B12, na madini ya chuma.
Vidonda hivi huwaathiri sana watu wengi na hutokea sana kwenye lips, ulimi , mashavu, kingo na kuta za meno ambapo pia huweza kusambaa hadi kwenye koromeo endapo havitatibiwa mapema.

Pamoja na kutembelea hospitali ambapo dawa kama za antibiotiki, fangasi, virusi na zile za kupunguza maumivu na uvimbe huweza kutolewa kulingana na ukubwa wa tatzo pia unaweza kufanya yafuatayo kujitibu nyumbani

  • Epuka vyakula na vinywaji vya moto au baridi sana kwani huchelewesha kupona kwa vidonda

  • Kunywa juice ya matunda mbali mbali itakayokuwezesha kupata virutubisho na madini ambayo huongeza kinga ya mwili

  • Kunywa maji mengi kila siku ambayo sio ya moto wala baridi

  • Piga mswaki mara kwa mara na taratibu ili kuepuka kukwangua na kutonesha sehemu zenye vidonda

  • Kula sana matunda asa machungwa, machenza na malimao kwani yana kiasi kikubwa cha vitamin ambayo huongeza kinga ya mwili. Pia yana asidi ambayo inaweza kuua wadudu wanaokuwepo mdomoni

  • Unaweza kununua pia Maltivitamini dawa yenye mchanganyiko wa virutubisho vingi ambavyo huweza kusaidia kurudisha kinga ya mwili katika hali ya kawaida

  • Kama vidonda vinaambatana na maumivu makali tumia dawa ya kutuliza maumivu au kuweka barafu ambayo hupunguza maumivu kwa muda

  • Tumia Asali ambayo husaidi kuua vimelea, kuponya makovu na kulainisha sehemu zenye vidonda pakaa asali kwenye vidonda asubuhi mchana na usiku.

  • Kunywa maji ya nazi(madafu) ambayo upoza mwili na huua wadudu hatari mdomoni sambamba na kupaka mafuta ya nazi kwenye kidonda ili kupona haraka.

Kumbuka vidonda visivyopona kwa muda zaidi ya wiki mbili vinaweza kuashiria tatizo kubwa na sugu mwilini hivyo inakupasa kufika hospitali ambapo utapewa dawa za bakteria, fungasi, virusi au dawa nyingine zozote kulinga na ukubwa na visababishi vya tatizo.
Usipo pona nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu.
 
Wakuu salaam,

Hili tatizo la kutoka vidonda mdomoni, lina miez sasa huwa natumiaga vitamin B12 huwa vinaondoka baada ya siku kadhaa vinarudi

Hasa vinatokea kwenye ulimi na lips, hadi kula nimekuwa mvivu jinsi vinavyouma, pia sometime vinaambatana na homa, fizi kutoa damu

Msaada wa mawazo dawa gani inaweza kumaliza hili tatizo ili niishi kwa amani naamini kuna madaktari humu

NB: mimi syo mpenzi wa kuzama chumvini na sijawahi

Sent from my GT-N8000 using JamiiForums mobile app
Nenda Hospital kafanye uchunguzi wa kina kuhusu hilo tatizo.
 
Kamauone daktari wa kinywa na meno kwa ushauri mzuri wa kitabibu lakini unawez pia kutumia "Medi oral solution " nidawa ya kusukutua kinywa,pamoja na "Daktarin oral Gel" Kwa upande wa fizi kutoa damu ni ishara kuwa kuna kitu hakiko sawa kinywani,take antibiotic to manage it,medicine like Ampicloxacillin ni dawa nzuri tu ,na kwa upande wa homa tumia panadol tu.
Narudia tena ,nenda hospital kamuone daktari wa kinywa na meno.
 
Opthous/stress ulcers
Zinatokea zinawasumbua wengi mainly mwili unakua hypersensitive
Use of anti hypersensitive kumodulate body immunity unafanya mzuri

Dr
 
Je kwa mtt mdgo wa miaka 2 anasumbuliwa na tatzo Hilo chanzo chake Ni nn Happ kwenye matatizo ya kinywa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom