Vidokezo (tips) kwa wanaotaka kujifunzakutengeneza apps

Jul 21, 2022
41
60
1. Kwanza kuwa mpole, wala usipanic code zikizinguwa, hii ni kawaida.

2. Usiwaze kutengeneza app kubwa saaanaau yenye mambo mengi mapema.

3. Kutengeneza app ni kama ujenzi, usiwaze saaana kwamba utamaliza lini.

4. Usiwe msiri kuuliza unapokwama na wala usiwe msiri kusaidia wengine. Hata hivyo jitahidi ku-struggle kidogo kabla hujauliza (ili uwe best programmer).

5. Pangilia vizuri codes zako, na weka comments ili kuweza kukumbuka dhamira ya codes hizo.

6. Majina ya variable, function n.k. yawe yenye kuleta maana, kwa mfano, function ya kutafuta umri usiandike get(){} bali iwe getAge(){} au calcAge(). Fupisha codes ila zilete maana.

7. Kukopi na kupesti codes kunakoruhusiwa ni kule ambako unakopi lakini unaelewa unachokikopi na unaweza kubadilisha hizo codes kulingana na mahitaji yako. Hivyo epuka kubandika codes za watu wengine bila kuzielewa.

8. App isikulazimishe ifanye inachotaka hiyo bali wewe ndo uilazimishe ifanye unachotaka.

9. Epuka kutumia external (third party) libraries au frameworks bila sababu ya msingi. Kumbuka hizi libraries zinachangia sana file la app yako kuwa kubwa sana.

- Yaani unaweka library (lib file) la 30 MB kwa ajili ya app yako ya 2 MB kwa lengo la kupata function moja tu ambayo hata wewe mwenyewe unaweza kui-code (hii haitakiwi).

kama una madini zaidi share hapo chini na wengine wajifunze
 
Back
Top Bottom