Suluhisho ni mabasi yatembee usiku kule ambako ni salama
Fikiria basi litoke Arusha saa moja/19h00 jioni na linatakiwa lifike dar saa kumi na mbili asubuhi (06h00)
Sana sana litaenda kms70 kwani watu wanahitaku wafike kumekucha
Huku Africa tuna poteza muda mwingi sana halafu tunalalamika kuwa Nchi ni masikini
Fikiria mabasi kama 450 yanatembea mchana mzima, ina maana tuna watu wazalishaji 27,000 kila siku wanakaa kwenye mabasi kutwa nzima; zidisha kwa mwezi na kwa mwaka???
Wanaotamani mabasi yakimbie ni wafanyabiasha na wanaowahi majukumu ambao wangesafiri usiku kwa raha zao. Mchana tuwachie wale wanaokwenda kusalimia