VIDEO - Vya Bure Gharama.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Vya Bure Gharama..

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  VIDEO - Vya Bure Gharama..
  [​IMG]
  Maelfu ya wapenzi wa soka wakisukumizana kuwania kuingia uwanjani kuangalia mechi ya Nigeria na Korea Kaskazini Monday, June 07, 2010 2:06 AM
  Jumla ya watu 14 wamejeruhiwa wakati maelfu ya watu nchini Afrika Kusini walipogombania kuingia uwanjani kuangalia bure mechi ya kirafiki kati ya Nigeria na Korea Kaskazini. Mechi hiyo ya kirafiki ilifanyika mjini Johannesburg kwenye uwanja wa Makhulong ambao una uwezo wa kuingiza watu 10,000 tu.

  Mechi hiyo ambayo kiingilio kilikuwa ni BURE ilivuta watu wengi sana kuliko uwezo wa uwanja huo.

  Wakati mageti ya uwanja huo yalipofunguliwa, polisi walizidiwa nguvu na maelfu ya watu walisukumizana kwa fujo kuwania kuingia ndani hali iliyosababisha watu wakanyagane na wengine kupoteza viatu na mali zao.

  Polisi walifanikiwa kuyafunga mageti ili kuepuka maafa zaidi lakini mageti yalipofunguliwa tena, polisi walizidiwa tena nguvu na kusababisha vurugu kubwa zaidi ya mwanzo.

  Katika patashika hilo, watu 14 walilazimika kupewa matibabu uwanjani baada ya kudondoka na kukanyagwa.

  Mechi iliendelea kama kawaida na Nigeria ilifanikiwa kuifunga Korea Kaskazini mabao 3-1.

  Magoli ya Nigeria yalifungwa na Aiyegbeni Yakubu, Victor Obinna na Obafemi Martins. Goli la kufutia machozi la Korea Kaskazini lilifungwa na Jong Tea-se.

  Chini ni VIDEO ya tukio hilo. Bonyeza hapa NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...