Licha ya faida zitokanazo na teknolojia hii katika uchaguzi lakini pia moja ya athari inayoweza kusababishwa na teknolojia ya akili unde ni uwezekano wa kuenea kwa taarifa potoshi.
Video na sauti za kughushi (Deepfake) zinazotengenezwa kwa Akili unde zinaweza kutumika kuwapotosha wapiga kura na kudhoofisha imani katika mchakato wa uchaguzi.
Deepfake zinaweza kumfanya mtu aonekane akisema au akifanya mambo ambayo hakuyafanya.
Tembelea Jukwaa la
JamiiCheck kupata uhalisia wa video iwapo imetengenezwa kwa akili unde au lah ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi kuelekea uchaguzi mkuu 2025.