Video: Morgan Tsvangirai akipanga kumuua Mugabe

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Hii ni video ya Miaka kama Tisa iliyopita ambapo Wazungu kadhaa walifanyia Mkutano London wakiwa na Morgan Tsvangirai kupanga Kumuua Mugabe! Kosa walimhusisha Kiongozi wa kijeshi ambaye alimstua Mugabe na Wakaanza Kufuatilia Nyendo zao!

Kadhalika Mugabe alimwomba Mwenyekiti wa AU, Rais Kikwete ambaye alituma satu Maalumu kwa spidi ya Radi Wiki chache kabla ya Uchaguzi wa Zimbabwe kuhakikisha hilo halitokei. Swali langu ni kuwa Kwa Ushahidi huu, technically kwanini Tsvangirai hakuguswa? Au ni Hekima ya Kikwete?

Morgan anashirikiana na wazungu

Yaani hapo wazungu wanataka ardhi na free market

Japo siungani sana na Mugabe ila kitendo cha kushirikiana na wazungu dah sasa ana tofauti gani na machief walioshirikiana na wakoloni kuuza watumwa,hao wazungu watamtumia tu huyo Morgan wakifanikisha lao kuingia mikataba ya kifisadi itakayoumiza nchi kwa karne kisha wanamtupa

Kwanini hakuguswa watajuana wenyewe labda Mugabe hakutaka kuingia kwenye machafuko zaidi na wazungu
 
Walikuwa na haraka tu , huyu atachukuliwa na Mungu mwenyewe tena wala si mbali , yanini kujichumia dhambi ?
Mugabe kwa sehemu ni Mbaya lakini kwa Sehemu ni Hero, Myama kwa kuuwa Wandebele waliokuwa Wakimsapoti Josua Nkomo, Na myama kwa kuchukua Arthi bila Mpangilio. Ila baada ya Uhuru ardhi yenye Rutuba kiasi cha 80% ilikuwa Mashamba ya Wazungu, Wazawa walikuwa pembezoni kwenye mawe na Maporomoko! Baada ya Uhuru Waingereza na Marekani waliingia Mkataba wa Lancaster na Serikali ya Mugabe kuwa watatoa Fedha ambazo zingetumika kununu mashamba asilimia Fulani Kutoka kwa wazungu na Kuwagawia Wazawa. Wakati wa Waziri Mkuu Tony Blair Mugabe akakumbushia Mkataba wa Lancaster na Kumwambia Blair kuwa Waliopigania Uhuru wanamsuumbua, Tony Blair akamjibu kunya kuwa hawezi kurithi maswala ya Ukoloni. Pia Tony Blair akiwa mtoto kwa Mugabe na Cheo cha Chini kuliko Mugabe Jumuia ya Madola! (Mugabe alitunukiwa knighthood) Akamwita Mugabe Stupid. Ndipo hasa Mugabe akaamua Amwonyeshe Utemi Blair akachukua Mashamba kwa nguvu, Blair akakimbilia kwa Bush Kumchomea Mugabe Utambi ndipo vikaanza Vikwazo vya Uchumi na Waliokuwa wakimwona Mwanasesere wao sasa wakaanza kumwita Joka!

robert-mugabe-01.jpg

Mugabe received Knighthood

article-2295626-18C6F51D000005DC-450_964x593.jpg

Mugabe Pia ni Jesuit, Ndio Maana hata aseme nini hawezi Kuguswa na Yeyote! Ni Makubaliano ya Siri Tangu Utawala wa Reagan! Pope hamwinamii Rais yeyote Duniani wanamwinamia wao Kasoro Mugabe peke yake!
 
Morgan anashirikiana na wazungu

Yaani hapo wazungu wanataka ardhi na free market

Japo siungani sana na Mugabe ila kitendo cha kushirikiana na wazungu dah sasa ana tofauti gani na machief walioshirikiana na wakoloni kuuza watumwa,hao wazungu watamtumia tu huyo Morgan wakifanikisha lao kuingia mikataba ya kifisadi itakayoumiza nchi kwa karne kisha wanamtupa

Kwanini hakuguswa watajuana wenyewe labda Mugabe hakutaka kuingia kwenye machafuko zaidi na wazungu

Uingereza walitegemea sana imports za Fruits na mbogamboga kutoka Zimbabwe, Mashamba ya Wazungu
 
Wazungu ni ndumilakuwili kweli yan..Sasa kwenye mipango nyeti km hiyo walikuwa wanarekodi ili iweje!???
 
Ili baadae Morgan angejifanya joroe kukaa juu baada mission wamkaange.
Na angekua akiwapinga wanamtishia hako ka recording mission talks
 
KAMA VIONGOZI WANGU WA CHADEMA ALIVYORECODIWA UGERUMANI KWA MAKUBALIANO FULANI NA IKATENGENEZWA NJIA YA KUMPOTEZA MSAIDIZI WA MWENYEKITI ILI NCH ISIMAME.BAADA YA KUBUNA SASA NASIKIA KUNATETESI MADEVU WA ZANJ NA MANYWERE MEUPE WANAFADHILI MAUAJI KULE PWANI..NASEMA NASIKIA NA KAMA NI KWELI JESHI LA POLISI LIFANYE KAZI YAKE

Ili baadae Morgan angejifanya joroe kukaa juu baada mission wamkaange.
Na angekua akiwapinga wanamtishia hako ka recording mission talks
 
Duuuuh
Africans are the greatest enemies to Africa
Walifanya the same thing na kina Sankara and Lumumba. May their Souls Rest in PEace!
 
Kwani Morgan yupo wapi kwasasa? Kwasababu sijamsikia kitambo
 
KAMA VIONGOZI WANGU WA CHADEMA ALIVYORECODIWA UGERUMANI KWA MAKUBALIANO FULANI NA IKATENGENEZWA NJIA YA KUMPOTEZA MSAIDIZI WA MWENYEKITI ILI NCH ISIMAME.BAADA YA KUBUNA SASA NASIKIA KUNATETESI MADEVU WA ZANJ NA MANYWERE MEUPE WANAFADHILI MAUAJI KULE PWANI..NASEMA NASIKIA NA KAMA NI KWELI JESHI LA POLISI LIFANYE KAZI YAKE
This is BS weka hiyo Video
 
Wazungu ni ndumilakuwili kweli yan..Sasa kwenye mipango nyeti km hiyo walikuwa wanarekodi ili iweje!???
Hawakujua Wanarekodiwa Mugabe alishtuliwa na Huyu Mwanajeshi xxx waliomhusisha kwa hiyo wakawaacha wafanye mkutano huku wakiwarekodi. Ujue Mugabe ni Jesuit ambao Asili ya Neno Majasusi limetokea Kwao, (believe me najua nachoongea oops) Biashara ya Ukachero wao wameifanya kwa Miaka karibu 800 wengine wote na Makeke yao wanajaribu!
 
Zimbabwe ina hali ngumu sana ya kiuchumi,na taifa lao limetumbukia katika ufukara wa kutupwa.
Tatizo huyo mzee ameishapoteza memory wanaoumia ni wananchi walio wengi.
Wazimbabwe wameikimbia nchi yao kwa mamilioni kwenda South Africa,its realy biggest tragedy kuliko hata ule uhuru fake waliopigania.Tuwaombee wana hali ngumu sana.
 
Tatizo wazungu wamekwambia hivyo kuwa kachuma dhambi na wewe bila kuchuja sababu walikutengenezea tv basi umeamua kuwaamini.
Ugomvi wangu na Mugabe hautaisha milele , ni kama ninavyopambana na ccm .

Huyu mzee tangu ajione mungu wa zimbabwe kwa kusigina katiba na kukandamiza wapinzani simtaki kabisa .
 
KAMA VIONGOZI WANGU WA CHADEMA ALIVYORECODIWA UGERUMANI KWA MAKUBALIANO FULANI NA IKATENGENEZWA NJIA YA KUMPOTEZA MSAIDIZI WA MWENYEKITI ILI NCH ISIMAME.BAADA YA KUBUNA SASA NASIKIA KUNATETESI MADEVU WA ZANJ NA MANYWERE MEUPE WANAFADHILI MAUAJI KULE PWANI..NASEMA NASIKIA NA KAMA NI KWELI JESHI LA POLISI LIFANYE KAZI YAKE
Uzushi wa kishamba kama huu utakusaidia nini ? Hivi mtaweza kumaliza haya mauaji kwa mawazo ya kibashite kama haya ?
 
Ugomvi wangu na Mugabe hautaisha milele , ni kama ninavyopambana na ccm .

Huyu mzee tangu ajione mungu wa zimbabwe kwa kusigina katiba na kukandamiza wapinzani simtaki kabisa .
Mbona dj humchukii kwa kusigina katiba ya chama?
 
Back
Top Bottom