VIDEO - Mechi Ambayo Haijawahi Kutokea Duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Mechi Ambayo Haijawahi Kutokea Duniani

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, May 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Athletic Bilbao walipochuana na timu ya vijana yenye wachezaji 100 Tuesday, May 25, 2010 2:44 AM
  Ilikuwa ni mechi ambayo haijawahi kutokea duniani, wachezaji 11 wa timu ya Athletic Bilbao waliingiwa uwanjani kucheza na timu yenye wachezaji 100 na magolikipa watatu. Mwisho wa mechi Bilbao walishinda 5-3. Washabiki 20,000 walikuwepo uwanjani kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa maalumu kwaajili ya kuchangia pesa kwa mashirika ya hisani na kumuaga mchezaji wa Athletic Bilbao Joseba Etxeberria, 32, ambaye anaondoka kwenye timu hiyo baada ya miaka 15.

  Timu ya Ahtletic Bilbao ikiingiza uwanjani kikosi cha mastaa wake wa ligi kuu ya Hispania walicheza kwa kutumia fomesheni yao maarufu ya 4-4-2 lakini timu pinzani yenye vijana 100 ilitumia fomesheni ya 20-60-17.

  Ilikuwa ni vigumu kuuona mpira upo wapi kutokana na msongamano wa wachezaji uwanjani na haijulikani ni wachezaji wangapi walifanikiwa kuugusa mpira.

  Pamoja na kwamba timu yenye wachezaji 100 ilikuwa na magokipa watatu kwenye lango lake, ilitoka uwanjani ikiwa imefungwa 5-3.

  Chini ni VIDEO ya mechi hiyo.


  VIDEO - Mechi Ambayo Haijawahi Kutokea Duniani  Kuiona hiyo Video bonyeza hapa NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mechi hii ndo haijawahi kutokea duniani? Aaah imetokea bwana si watu wamepiga game! Sema game iliyochezwa na watu wengi zaidi, na ilikuwa ya kujfurahisha tu, but akhsante kwa kuimuvzisha hapa
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Duh mbona huku kwetu uswazi hua inatokea sana tu chandimu
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,254
  Trophy Points: 280
  Swadakta
   
Loading...