Nimeangalia ile picha Msigwa aliyopost twitter, ni ya mwaka 1987 lakini kwa situation na pamba alizokuwa anapiga ni wazi si mtu wa kubeza na kumlinganisha na wajamaa wengi walioibuka katika siasa za hivi karibuni.
Inaelekea Msigwa ALIJITAMBUA siku nyingi na sidhani kama ubunge kwake ndio mwanzo au mwisho wake, same to Mh. Sugu.
Ukitaka kuelewa ninachoongea hebu waulize wanasiasa wengi wenye umri wa miaka 45 kwenda chini huo mwaka wa 1987 watuonyeshe nao picha zao walikuwa wapi na wanafanya nini ndipo utakubaliana nami!