Video: Je, IGP Sirro anapuuzwa na RPC Muroto?

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
Wakuu kama mnavyofahamu siku za nyuma kidogo IGP aliansa semina elekezi au kikao kazi na makambda wote wa mikoa ya kipolisi Tanzania.
Katika hicho moja ya mambo aliyosisitiza ni maRPC kutowahukumu watuhumiwa hadharani mfano afanyavyo kamanda Muroto wa dar na kusisitiza hao ni watuhumiwa tu.

Lakini baada ya maelekezo hayo naona hali haijaeleweka kwa kamanda MUROTO wa Dodoma kwani Leo ametoa video nyingine akidhalilisha mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wa benki mkoani Dodoma, mbele ya kamera na waandshi wa habari.

My take:
JE, KAMANDA MUROTO ANMDHARAU/HAMTII/AMEMPUUZIA BOSI WAKE??
NA HII KIMEDANI/KIJESHI IMEAKAAJE?
VIDEO HUSIKA NIMEAMBATANISHA.
 
Attachments

  • 72631055_166300134428008_7660419006390448555_n.mp4
    3.9 MB
Ramli chonganishi hizo mbona yeye siro mwenyewe akikamata anawaonyesha ..sasa bila kuonyesha hivyo atakubalikaje katika jamii na unajua saa hivi kazi inafanywa kwa sifa ili angalau upate ka cheo
 
Ramli chonganishi hizo mbona yeye siro mwenyewe akikamata anawaonyesha ..sasa bila kuonyesha hivyo atakubalikaje katika jamii na unajua saa hivi kazi inafanywa kwa sifa ili angalau upate ka cheo
Ila bosi wake si alisha mkataza! Kwanini hamuheshimu?
 
Mzee huyo ndo anafanya kazi, Sirrro ndo mtu wa siasa ila anajifanya kutuzunguka tumuone anasimamia maadili ya jeshi la polisi kumbe hamna kitu
 
Bila shaka muda si mrefu atatangazwa kuwa bosi mpya wa mapoti wote nchini. Inawezekana huyo bosi wake wa sasa, ameshahisi kitu na ndiyo maana hata hiyo siku aliwatolea povu la kutosha hao wasaidizi wake kwa namna wanavyo kimendea cheo chake.
 
Wakuu kama mnavyofahamu siku za nyuma kidogo IGP aliansa semina elekezi au kikao kazi na makambda wote wa mikoa ya kipolisi Tanzania.
Katika hicho moja ya mambo aliyosisitiza ni maRPC kutowahukumu watuhumiwa hadharani mfano afanyavyo kamanda Muroto wa dar na kusisitiza hao ni watuhumiwa tu.

Lakini baada ya maelekezo hayo naona hali haijaeleweka kwa kamanda MUROTO wa Dodoma kwani Leo ametoa video nyingine akidhalilisha mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wa benki mkoani Dodoma, mbele ya kamera na waandshi wa habari.

My take:
JE, KAMANDA MUROTO ANMDHARAU/HAMTII/AMEMPUUZIA BOSI WAKE??
NA HII KIMEDANI/KIJESHI IMEAKAAJE?
VIDEO HUSIKA NIMEAMBATANISHA.
Pitia vizuri uzi wako kuna Muroto wa Dar na Muroto wa Dodoma.
 
Hiyo kuwaonyesha watuhumiwa ilikuwepo tangu enzi za kina Alfred Gewe. Muroto siyo wa kwanza
Sio kila mtuhumiwa anatakiwa kuonyeshwa kwenye. Vyombo vya habari, kuna vigezo. Vyake, na iweje kati ya ma RPC, wote,huyu tu ndio anapenda sana. Kufanya hivyo?
 
IGP si anaweza tuu kumbadilisha pale na kumuacha msimbazi central awe anasoma magazeti?
 
Back
Top Bottom