- Tunachokijua
- Wadau wa JamiiCheck kutoka katika jukwaa la JamiiCheck.com na kurasa za mitandao za JamiiCheck wameshiriki kubainisha dosari zinazoonekana katika video iliyowasilishwa na mdau.
Ambapo wengi wamebainisha kuwa video hiyo si halisi na kuna uwezekano kuwa imetengenezwa kwa Teknolojia ya AKili Unde (AI) kutokana na sababu zilizotajwa ambazo haziakisi uhalisia wa mazingiraya kawaida.
Uhalisia wa video
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde.
Licha ya mapungufu ynayoonekana katika video hiyo ikiwemo watu kufanya matendo yasiyo ya kawaida lakini pia nyenzo za kidigitali za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa AI, yanabainisha kuwa maudhui hayo yametengenezwa kwa teknolojia hiyo.
Nyenzo ya Hive Moderation inaonesha kuwa Asilimia 99 za video hiyo imetengenezwa kwa teknolojia hiyo.