chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Kwenye nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kati ya nchi ambazo zilikuwa zina afadhali kwenye demokrasia ni Kenya na Tanzania,
nchi hizi tunadhani zinapiga hatua kwenye demokrasia na utawala bora lakini sio, zinaenda hatua mbili mbele kisha zinarudi hatua tatu nyuma
Tanzania kwenye awamu ya 4 tuliona kuna uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza, wapinzani wakawa wanaheshimika mawazo yao, hata rais Kikwete akamchagua mbunge wa upinzani James Mbatia kati ya wabunge wa kuteuliwa, daftari la wapiga kura likaboreshwa, uchaguzi wa 2015 ukafanyika kwa uwazi mkubwa na watu wengi kujitokeza kupiga kura,
lakini kwa awamu hii tumeona kuna dalili za kuanza kurudi kule na hii improvement kidogo tuliyoonyesha ikapotea yote, tumeona wanasiasa wakubwa wakiuawa mfano Alphonce Mawazo yule mwenye kiti wa Chadema mkoa wa Geita, pia kuna diwani wa upinzani aliuawa huko Kagera na serikali haikuonekana kukemea kama ilivyopaswa
kwa Kenya baada ya vurugu za uchaguzi nchi hii ilikuwa stable, uchaguzi ukafanyika 2012 uliokuwa stable tukadhani kuwa nchi hii imeshastaarabika na sasa mambo yatakuwa yana boreka hatua kwa hatua hadi kufikia utawala safi wenye haki kwa kila raia lakini haya maandamano yanayofanyika kutaka tume ya uchaguzi ibadilishwe na polisi kutumia nguvu na ukandamizaji mkubwa kudhibiti maandamano hayo inatoa picha kuwa bado tuna safari ndefu ya kwenda