Vicoba ni mradi wa kweli?!

mavado

JF-Expert Member
Jun 25, 2014
1,153
794
Mambo vp waungwana, naomba kuuliza hivi hii habari ya viccoba saccoss ina ukweli kiasi gani, kupata mkopo ndani ya dakika 55, tujuzane wenye kujua..
 
Wezi hao utaibiwa,halafu kama wana dawa,ukipiga sim utajikuta umeingia kichwa kichwa.
Wamelizwa watu kibao kutuma pesa kwa mobile transfer
 
Nnavojua mimi vikoba ni kikundi cha watu waliojiunga pamoja, wanaotoa hisa kila wiki then baada ya mda flani wanafundishwa ujasiria mali na wanakopeshana kulingana na hisa ambazo unazitoa mimi vimenisaidia sana ivi vikoba nimeweza kuwekeza hisa zangu na kukopa kwa riba nafuu ya 10%.
 
10% kwa muda gani?

ndugu yangu Tabby riba ya 10% inaanzia miezi 6 hadi 12.. vikoba ni mkombozi kwa wasomi ambao hawajapata ajira. mie ni shuhuda wa hili jambo nilikuwa kapuku kila siku nalalamika gemu gumu lakini haa nashukuru sasa namiliki biashara..
 
Last edited by a moderator:
mkuu vikoba vingi huwa ni mwaka mmoja kwa riba ya 10% kwakweli nawashauri jiungeni huko zamani ilikua akina mama sasaivi na akina baba pia wapo nani mkombozi hasa
 
Samahani kiongozi sijaelewa. Unalipa riba ya asilimia kumi kila muda gani? Kila miezi sita, kila mwezi ama kila miezi 12?

Sijaelewa kwa kweli.

ndugu yangu Tabby riba ya 10% inaanzia miezi 6 hadi 12.. vikoba ni mkombozi kwa wasomi ambao hawajapata ajira. mie ni shuhuda wa hili jambo nilikuwa kapuku kila siku nalalamika gemu gumu lakini haa nashukuru sasa namiliki biashara..
 
Taby hayo yanaitwa marejesho kulingana na mkopo uliochukua mfano nimechukua 5m kwa riba ya 10% natakiwa nilipe ndani ya mwaka means kila mwisho wa mwezi napigiwa mahesabu na kutakiwa kupeleka hayo marejesho il ndani ya mwaka mkopo uwe umeisha na unapochukua mkopo wanakata riba kabisa
 
Vocoba vinasaidia sana kwa mikopo midogo

Anazungumzia FOCUS VICOBA wale matapeli wa
kutumia mtandao. Mara nyingi wanaposti matangazo kwa kutumia akaunti za mitandao ya kijamii za watu maarufu kama Halima Mdee, Zitto, Lowassa, Diamond, Mpoto, Millard na wengineo. Epukaneni nao ni matapeli..!
 
Back
Top Bottom