Nimekuwa nikifuatia mada hii tamu na ningependa kuchangia mawazo kidogo hapa.
Mimi ni stronger believer wa democracy na market economy, ila niko against na western liberal democracy na western market economy, na kwa mtazamo wangu Africa haitaondokana na umasiki kamwe kama itaendelea kukumbatia liberal democracy na market economy iliyokuwa designed na western countries...nafafanua.
Democracy tuliyonayo sasa Tz na Africa kwa ujumla ni ile tuyorithi kutoka kwa wakoloni na sasa wakoloni hawa wamekuwa waki-imodify democracy hii kadri watakavyo na huku sisi tukiimbiza na kwenda na mabadiriko hayo pasipo kujali utofauti wetu na west. Kwa maana nyingine tunajikuta lazima tukimbie kabla hatujaanza hata kutambaa. Matokeo yake ni umasikini husio kifani.
Liberal democracy inafanya kazi west sio kwasababu ya uongozi imara wa west, wala sio kwasababu ya uchumi imara. Kwa sababu nature ya west ina support liberal democracy. Tofauti na Tz au nchi nyingine za Africa zilizokuwa na mfumo wa socialism uliokuwa na umuhimu katika kuyaunganisha makabila na watu wa dini/imani mbalimbali, nchi za magharibi hazina makabila, na hivyo partisan haiwi affected na ukabila bali na sera za chama husika. Tz na Africa tuna political culture tofauti na nilazima tuende kwa uangalifu sana katika kui-shape democracy tunayoiona inafaa. Congo, Sudan, Iraq, Burundi, Rwanda, Uganda, Somalia, na kwingineko tumeona liberal democracy inavyochukuwa sura ya shetani na kusababisha umwagaji wa damu. Kwanini??? Kwasababu democracy sio zaidi ya jumuisho la dini, ukabila, social class, na maisha ya kila siku ya binadamu. ...Hivyo basi demokrasia ya magharibi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wetu,,,tunatakiwa tuirekebishe democrasia hii ili ichukuwe shape ya tamaduni zetu, mila zetu, imani zetu, makabila yetu na kila kitu kinacho affect uzalishaji nk.
Markert economy: Market economy ilikuwapo Tz na Africa kwa ujumla kama ilivyokuwa democracy kabla ya wakoloni. Wakati ule mbuzi alikuwa anabadirishwa na gunia la mpunga at a price determined by the market. Kukiwa na mavuno mengi ya mpunga, mbuzi alikuwa anabadirishwa kwa magunia kadhaa, kukiwa na mbuzi wengi basi mpunga ulikwa na thamani na hivyo gunia la mpunga lilikuwa lina command karibu zizi zima la mbuzi. Hizi ni forces za supply na demand ambazo wachumi wa sasa wanajidai kutuletea Tz na Africa, wakituambia kwamba ni magic forces katika allocation za resources.
Sasa tunapokumbatia liberal makert economy mana yake tunakumbatia na upumbavu wake, ambao ni assumption kwamba kila kitu kina market value, na kwamba market value hii ni bora kuliko social value. Mfano, nchi za magharibi ukiunguliwa nyumba yako moto, jirani yako na familia yako wote wanafurahia, na hakuna atakayekupa pole? Kwanini?? Kwasababu moto ulionguza nyumba yako tayari una market value, ambayo ni bima ya nyumba. Sasa sisi waTz nyumba inapoungua ndio kwanza jamii inapoungana na wewe katika kuhakikisha unapata makazi, huu ni wakati ambao social fabric zinaunganishwa katika kuleta maendeleo ya jamii....Sasa tunapokumbatia liberal market economy manake social values ambazo ni muhimu katika kuleta huduma za jamii na upendo katika jamii zinamong'onyoka.
Matokeo yake, mwenye bima ndio atapeleka mtoto shule,,,,kama huna bima na unazeeka basi ni bora mtoto wako abaki nyumbani akuletee kuni, mana mtoto wako sasa ndio bima yako,,,,jamii iliyotakiwa iwe bima imekumbwa na liberal market economy inayosema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!!
Liberal market economy haikujali kama wewe huwezi ku-affect market, kadhalika liberal democracy haikujali kama wewe huwezi ku-convince. Hitimisho ni kwamba vitu hivi viwili lazima viangaliwe kwa undani zaidi ili kupata aina ya democracy na market economy inayotufaa watanzania.