Vibali vya Ujenzi Mbeya Mjini

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,922
5,619
Kuna urasimu mkubwa katika kupata kibali cha ujenzi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Kuna mfanyakazi anadai rushwa na kibali hatoi hata pale hiyo rushwa inapotolewa. Katika dunia ya leo, haiwezekani kibali kisitolewe zaidi ya miezi 3 baada ya mteja kulipia tozo stahili. Hili linapunguza mapato ya Halmashauri na kuhamasiha watu kujijengea utamaduni wa kujenga bila kufuata taratibu.

Takukuru Ofisi ya Mkoa fanyeni kazi yenu. Usalama wa Taifa hii nayo ni kazi yenu. Washughulikieni hawa watu. Sio kila kitu mpaka Rais au Waziri awaambie. Maofisa wanaohusika na utoaji vibali katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya ni vichomi sana. Mbona sisi wengine ni watumishi wa serikali kama wao na hatudai rushwa na kazi zinaenda vizuri?

Wadau ambao mmefanikiwa kupata vibali vya ujenzi Jiji Mbeya naombeni uzoefu wenu na suluhisho kwa tatizo hili.
 
Ni halmashauei nyingi sana wanatabia hizo za kutaka rushwa, ukienda hata kwenye halmashauri za jiji la Dar napo ni shida kabisa, bila rushwa hawatoi huduma
 
Back
Top Bottom