Vibali vya kurejea Utumishi wa Umma batch ya sita

Posho City

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
648
416
Wadau salaam kwenu!!!

Utumishi huwa kuna utaratibu wa watumishi wa umma waliofutwa payroll na baadae kupata kazi sehemu nyingine kuomba vibali kwa katibu mkuu kiongozi.

Kuna utaratibu unafanywa na mtumishi huyo anapewa kibali cha kurejea au anakataliwa.

Hapa naomba kujuzwa maana majina ya waombaji yanatolewaga kwa awamu(batch),kuna batch ya sita ilitoka tangu mwezi October,2015.

Je, kuna mhusika yeyote wa hili hapa yupo katika batch hii na amepata barua?Nipo huku mkoani lakini kila nikienda kwa mwajiri wangu wa zamani ambako ndo waliniambia barua itatumwa naambiwa bado.Naomba kujulishwa.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu hapo kuna mkuu wa idara hiyo room number 4c ni tatizo kabisa anaitwa Gibson Mayala, anakawaida ya kukalia taarifa na mafile ya watu bila sababu.
 
Kwa kasi ya Magufuli jaribu kufatilia sehemu zote tatu kwanza Utumish penyew then kwa Mwajiri WA zamani then kwa mwajiri mpya utapata majibu
 
Hapo hakuna rangi utaacha ona,kuna ndugu yangu alisumbuliwa na hii ishu kama miaka mitatu,ikabidi aende private sector tu.ila na nyie mjifunze,punguzeni tamaa,mkipata kazi serikalin muwe mnatulia kuepusha matatzo yasiyokua ya lazima.
 
Ndugu zangu ahsanteni.....Kibali kimepatikana na nimekubaliwa kurudi serikalini.....swali langu kwenu mnaojua hili.......Kibali kimeandikwa kuwa nilitoa notice ya 24hrs kbla ya kuacha kazi.....wakati sikufanya hivyo.....
Je....wakurugenzi hawa wa siku hizi ingawa kibali hiki toka kwa katibu mkuu kiongozi kinampa maekekezo mwajiri wangu wa zamani ahamishe cheki namba yangu kwenda kwa mwajiri wa sasa....je huyu mkurugenzi hawezi kataa kisa sikutoa notice hyo???
Au lzma atekeleze maagizo ya juu???
Kibali hiki nimekipata baada ya mchakato wa miaka 2 na vetting juu
 
Mkuu nipe procedure
 
Back
Top Bottom