Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Sheria huundwa kwa utaratibu maalum. Kuanzia katiba,sheria zitungwazo na Bunge, Kanuni, Waraka na Viapo huundwa kwa taratibu za kisheria. Ndiyo kusema, hakuna kiongozi yeyote wa kiserikali anayeweza kubuni Sheria kinyume na taratibu zilizopo.
Natambua,kama mkazi wa Dar es Salaam,kuwa waweza kubuni mambo mbalimbali katika kuboresha maisha ya wananchi. Ulibuni PF3 kuwa hospitalini na hata walimu kupanda bure kwenye daladala. Leo umeibuka na mpya kwa kuwaapisha watendaji wa jiji la Dar es Salaam.
Kwakuwa siifahamu Sheria yoyote inayosimamia viapo vya watendaji mbele ya Mkuu wa Mkoa,naona viapo hivyo kama ubunifu wa sheria kwakuwa viapo ni sheria. Halafu,viapo vya leo vina ahadi hadi za makosa ya kijinai.
Mkuu wa mkoa ni mtekelezaji na msimamizi wa sheria. Si mtunzi wa sheria. Kimsingi,namuasa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kubuni mambo yote mazuri lakini si kubuni sheria. Viapo vya leo,kama havisimamiwi na Sheria yoyote,havina nguvu yoyote ya kisheria.