Ventilation on MCC move is primed on wrong assumptions

Mkuu upo wodini?
 
anguko gani wewe.. hakuna kitu kama sisi kua kama DRC. ni vema tu kuepuka mtego wa hizo hela za MCC ii. usifikiri unaweza kuingia kwenye 18 za wamarekani ukaruka viunzi. MCC1 ilikua poa hii ya pili ni mtego. ila nachokubali ni diplomacy yetu kuonyesha kiwango. tusionekane wakorofi na uncle tom ili tuwe mtaani/vijiweni kwa amani.
 
Ushauri wangu kwa Rais Magufuli.
Hatukumchagua Rais ili aende kutunishiana misuli na wahisani au kupambana na ukoloni mamboleo.Tumemchagua ili tupate ajira, elimu bora,huduma nzuri za afya na miundo mbinu bora.
Tunaomba serikali ya awamu ya tano iache ubabe maana tutakaoumia ni sisi wananchi wa kawaida.Afanye diplomasia.Turudi mezani kufanya majadiliano.Watanzania hatutaki kufunga mkanda kwa sababu ya wazimu wa Jecha.
Naunga mkono wazo la Mufuruki.
 
Kikwete si ndio chanzo cha yote haya.
Huu sasa ndio unafiki.
JK akiwa rais na mwenyekiti wa CCM jecha ndio alifuta uchaguzi,Huyu mwingine kaingia kakuta tatizo lipo.

Acha unafiki.

Ahaa, ndiyo maana Magufuli akasema hayamuhusu?

Nnauhakika lugha imekupiga chenga usingekuja na utumbo kama huu.
 
Ningeshangaa kama bepari na nabii wa utajiri angeandika tofauti na haya. Hizi ndizo gharama za kuwanyenyekea wazungu kana kwamba Mungu wao ni mwingine.
Wewe mzee muda mwingine bora ukae kimya ulinde heshima yako ,ina maana yote aliyo andika hapo ni swala la kuwanyenyekea wazungu ? Hebu rudi soma tena ,hivi wewe unaweza kumkosoa Magufuli baada ya kukusifia ??
 
Jamani hata Ulaya hari ni ngumu. Washikiriwa bango na wanachi wao. Kukata misaada inasemwa sana huku. Kwahiyo siyo ajabu ukisikiya nchi nyingi zinjitowa.
Dunia imebadilika inabidi tubuni mbinu za kujisaidiya wenyewe.
" They need us as we need them".
 

Waliosusa ni MCC, weye mbona unakimbilia donors ebu soma tena. Hata marekani kuna mashirika mengi Zaidi ya MCC wengine wako site kazi zinaendelea.
 
Mkuu nje ya Mipaka yetu tunatambulika kama TANZANIA, hakuna Zanzibar, Mbeya wala Morogoro, Kosa la Zanzibar ni la Tanzania nzima.
 
Ni uchambuzi na ushauri mzuri sana kwa viongozi/watawala. Na hapa ndipo watu wanaposhindwa kujua ikiwa madhara ya MCC ni kukosa fedha pekee, au kutengeneza "mgogoro" wa kimahusiano?

Na pia tukumbuke kuwa sisi jama Tanzania kamwe hatuwezi "kuzuia" Maslahi/Interests za Marekani. Hivyo kudhani kuwa kujiwekea mazingira ya "waende zao" sio anuani ya kuzuia interests za hawa watu. Tusiingie huko. Tujipange kujenga uchumi wetu huku tukiendeleza mahusiano mema na watu hawa japo tunajua ni "urafiki wa mashaka".
 
..learn to see justice takes its course, crime remains to be crime with no regard of time, even if it takes 100 years to be revealed!
 
Mkuu nje ya Mipaka yetu tunatambulika kama TANZANIA, hakuna Zanzibar, Mbeya wala Morogoro, Kosa la Zanzibar ni la Tanzania nzima.

Wanajua uhuni tu wangekuwa hawajui MCC wangesema kuna tatizo la kura za nchi ya Zanzibar ya uchaguzi wa Raisi NA WAWAKILISHI?
 
Wanajua uhuni tu wangekuwa hawajui MCC wangesema kuna tatizo la kura za nchi ya Zanzibar ya uchaguzi wa Raisi NA WAWAKILISHI?
Ni kweli lakini huwezi kuitenga Zanzibar na Tanzania, kwa sababu hiyo ni sehemu ya JMT, sasa kama sehemu ya nchi imeharibu adhabu ni kwa nchi, sio rahisi kuweka vukwazo kwa Zanzibar, nadhani katiba yetu ndio ina shida.
 
Mawazo yake yaheshimiwe ila tusisahau kuwa naye alinufaika na udhalimu uliopita na pia alichangia kuua Shirika letu la ndege. ..Historia itamuhukumu. ..
Huu uzalendo unatokana na wasiwasi wa kwamba biashara zake zitakwama kwa namna moja au nyingine kutokana na maamuzi haya..kilio cha mamba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…